February 28, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mil 180 zachangwa leo kusaidia waathirika ajali MV Nyerere

Spread the love

MPAKA kufikia saa 12:00 jioni ya leo tarehe 23 Septemba 2018, jumla ya Sh. Mil 180 zimechangwa kwa ajili ya kusaidia walioathirika kwenye ajali ya MV. Nyerere. Anaandika Mwandishi Wetu … (endelea).

Wadau waliotoa michango hiyo mpaka sasa ni Vodacom (Mil 10), Tigo (Mil 150), Azim Dewji (Mil 10) na Waislam jamii ya Shia (Mil 10).

Pia michango mingine imeendelea kutolewa ikiwa ni pamoja na katoni za maji zaidi ya 6,000.

Serikali leo imefungua akaunti maalum kwa ajili ya kuchangia waathirika hao. Akaunti hiyo ni ‘Maafa ya MV Nyerere 31110057246 Tawi la MNB Kenyatta, Mwanza.’

Wadau hao wametoa michango hiyo leo katika Kisiwa cha Ukara ambapo ajali hiyo ilitokea Septemba 20, Mwaka huu.

Jenister Muhagama, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu akizungumza katika Kisiwa cha Ukara amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella kuhakikisha fedha hizo zinatumika kwa waathirika.

Amesema, ofisi yake itakuwa inaikagua akaunti hiyo mara kwa mara ili kuhakikisha malengo mahususi yanafikiwa.

Na kwamba, akaunti hiyo itasimamiwa na kuratibiwa na kitengo cha maafa cha Mkoa wa Mwanza.

error: Content is protected !!