August 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mikopo ya Halmashauri kutolewa kwa mtu mmoja mmoja

Dk. Festo Dugange, Naibu Waziri Ofisi ya Rais

Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania imesema inafanya tathimini ya kuangalia uwezekano wa kutoa mikopo ya Halmashauri kwa mtu mmoja mmoja. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Kwa sasa mikopo ya Halmashauri ambayo huwa ni asilimia 10 ya mapato ya ndani hutolewa kwa vikundi vya wanawake na vijana na kwa mtu mmoja mmoja kwa upande wa walemavu.

Akijibu maswali ya wabunge leo Jumatano tarehe 29 Juni, 2022, Naibu Waziri wa TAMISEMI, Festo Dugange, amesema uzoefu unaonyesha mikopo hiyo ina changamoto nyingi ikiwemo uwepo wa vikundi na mtazamo tofauti katika ufanyaji biashara na hivyo kuleta changamoto katika ukusanyaji na ufanisi wa mikopo yenyewe.

“Tunafanya tathimini ili uona uwezekano wa kukopesha mtu mmoja mmoja anayeweza kufanya shughuli zake mwenyewe ili kuongeza ufanisi katika maeneo hayo,” amesema Dugange.

Amesema baada ya tathimini hiyo itawawezesha kutengeneza kanuni itakatyoendana na Sheria ili kuanza kutekeleza utaratibu wa mikopo kwa mtu mmoja mmoja.

error: Content is protected !!