Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Mikopo ‘kausha damu’ yakausha unyumba Kinyerezi, Serikali yaingilia kati
Habari Mchanganyiko

Mikopo ‘kausha damu’ yakausha unyumba Kinyerezi, Serikali yaingilia kati

Spread the love

TANGU kuanza utaratibu wa baadhi ya wananchi kukopa mikopo ambayo mingine imegeuka kuwa ‘kausha damu’, changamoto nyingi zimeibuliwa ikiwa ni pamoja na kuvunjika kwa ndoa na baadhi ya familia kusambaratika. Anaripoti Marry Victor…(endelea).

Katika kuikabili hali hiyo, uongozi wa serikali ya Mtaa wa Kichangani Kata ya Kinyererezi umechukua jukumua la kulipa baadhi ya mikopo hiyo wanayodaiwa baadhi ya familia (wanawake) kwà lengo la kurudisha utulivu kwa baadhi ya familia.

Haya yanafanyika baada ya kuibuka kwà malalamiko kutoka kwà baadhi ya wazee walioshiriki katika kikao cha ndani kilichoitishwa hivi karibuni na Mwenyekiti wa Mtaa huo, Leonard Nyukuli kujadili hali ya ulinzi na usalama katika mtaa huo

Kwa mujibu ya Nyukuli katika kikao hicho alizungumza na wazee ambao baadhi yao kwa umri walionao tayari wamepoteza fursa ya kukopa.

Amesema; “Suala la wazee lipo tofauti na kausha damu kwà sababu wazee kwà umri wao hawakopesheki, niliozungumza kulingana na umri wao hawakopesheki.

“Nami nilizungumza nao mapema kwà ajili ya kujadili hali ya ulinzi na usalama katika eneo letu la Kichangani. Wao walieleza baadhi ya vitu na mimi nilieleza baadhi ya vitu. Baada ya hapo tukakubaliana mambo ha ulinzi shirikishi tuje kuzungumza katika mkutano wa wananchi wote ambao utaitishwa hivi karibuni,” amesema.

Nyukuli ametaja mafanikio yaliyopatikana baada ya wananchi kujitolea kulinda nyakati za usiku kwamba mtaa wake umejitahidi kwani uhalifu uliokuwa unatokea kwà mara kwa mara sasa umekoma.

“Hakuna mtu anayeamka asubuhi na kulalamika kuibiwa televisheni au chochote ndani ya nyumba yake, wananchi wanajitoa kwà kiwango kikubwa kuhakikisha wanaimarisha ulinzi,” amesema.

Kikao pia kilijadili mafanikio katika kipindi cha miaka minne kuhusu suala la maji, kupitia tamko la aliyekuwa Rais awamu ya tano Dk. John Magufuli wakati anaomba kura kipindi cha pili katika mkutano uliofanyka viwanja vya Kecha, alitoa maelekezo kwamba anataka kuona eneo la Kinyerezi na Kifuru maji yakipatikana.

“Katika hili, usambazaji maji kila kaya unaendelea. Sina takwimu sahihi zinazoonesha ni kaya ngapi zimekwisha patiwa maji lakini ninachoweza kusema maji safi na salama yanapatikana Kinyerezi na maeneo mengine,” amesema.

Akizungumzia kuhusu changamoto inayotokana na mikopo ya fedha, Mwenyekiti huyo ameongeza kuwa:  “Wananchi walikuwa na matumaini makubwa ya kupatiwa mkopo na halmashauri  lakini mpaka sasa mikopo hiyo imekuwa ni changamoto, haiwafikii wananchi kama ilivyotangazwa.

“Awali mikopo huo ulikuwa ukiombwa kupitia halmashauri lakini kwà sasa mfumo umebadilika wanaomba kupitia mtandao lakini bado katika mtaa wa Kichangani tangu mikopo hiyo inanze vikundi vilivyofanikiwa kupata mkopo huo ni vitatu tu. Kwà hiyo ndani ya miaka minne hiii hakuna kikundi chochote kilichopata na ndio sababu inayowasukuma baadhi ya wananchi wanafanya maamuzi ya kukopa kausha damu.

“Wananchi wanakopa mikopo katika taasisi zinazoumiza ambazo zinataka rejesho la mkopo lilipwe kila siku. Kwa mfano mtu anahitajika akope kiasi cha Sh 100,000 na kutakiwa kila siku urejeshe Sh 4,500 kwà hiyo kwà mwananchi wa kawaida pamoja na kwamba alikuwa na lengo zuri la kukopa lakini mwisho wa siku anashindwa kabisa.

“Nimepokea malalamko na kesi nyingi katika ofisi yetu na mengi ya malalamiko hayo ni watu kushindwa kulipa mikopo ya kila siku. Tumeziomba baadhi ya taasisi zinazotoa huduma hizo ikiwemo Twangawima Microfinance watuandikie barua ya kuona namna gani tunaweza kushughulikia suala hilo ikiwezekana hata ofisi kuingia gharama na kuamua kulipa mikopo hiyo ambayo ni kiasi cha Sh milioni moja. Hiki ni kiwango cha mkopo wanachodaiwa wananchi sita katika mtaa wangu.

“Uamuzi huu utasaidia maana katika kikao hicho nimepokea pia malalamiko ya kulegalega kwa ndoa nyingi, malalamiko ni kwamba kina mama hawatoi unyumba kutokana na vichwa kuzongwa na madeni, hakuna utulivu katika familia. Hivyo, ofisi imejipanga kuhakikisha amani na utulivu unarejea katika baadhi ya familia,” amesema.

Awali akizungumza na Mwandishi wetu, Mjumbe wa nyumba 10, Zudeda alisema wazee wamelalamika kwamba hakuna tena utulivu katika kupata tendo la ndoa.

“Mikopo imewasababisha akina mama hawatulii majumbani. Unyumba hawapewi muda mwingi kina mama wanafikiria wapi wanapata marejesho. Hivyo ofisi imeamua kuingilia kati.

Mmoja wa wananchi ambaye naye ni miongoni mwa wanaodaiwa amesema kitendo cha kushindwa kulipa marejesho ya kausha damu ni kutokana na hali ya kifedha kuwa ngumu zaidi.

“Umefika wakati hatuwezi kulipa tena marejesho. Ukiamua kulipa ina maana huduma za nyumbani ikiwemo kuhudumia watoto angalau kupata mlo mmoja wa mchana haiwezekani tena” alisema mwananchi huyo aliyomba hifadhi ya jina.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!