May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mikoa inayoongoza kwa malaria yatajwa, waziri atoa maagizo

Spread the love

HALMASHAURI 61 kutoka katika mikoa sita ya Tanzania Bara, imetajwa kuongoza kwa kuwa na mamabukizi ya ugonjwa wa malaria. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Akifunga kilele cha maadhimisho ya siku ya Malaria duniani, leo Jumatatu, tarehe 25 Aprili 2022, jijini Dodoma, Waziri wa Afya, ameitaja mikoa hiyo kuwa ni Kigoma, ulioshika namba moja kwa kuwa asilimia 24 ya maambukizi. Geita na Kegera (17%), Mtwara (15%), Lindi na Ruvuma (12%).

Ummy amewaagiza watalaamu wa afya kufanya utafiti ili kubaini kwa nini mikoa hiyo ina idadi kubwa ya maambukizi ya ugonjwa huo.

“Na mimi niwape changamoto watalaamu wetu wa utafiti, kwa nini mikoa hiyo ndiyo ina idadi kubwa ya wagonjwa wa malaria. Ni kwa sababu ya matatizo ya hali ya hewa, changamoto za kijiografia au ni nini? Tuje na majawabu ya kisayansi kwa nini Malaria iko kubwa katika mikoa hiyo sita ya Kanda ya Ziwa,” amesema Ummy.

Aidha, Ummy ametaja mikoa yenye kiwango cha chini cha maambukizi ya ugonjwa wa Malaria, ambayo ni Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Njombe na Iringa.

Waziri huyo wa afya amesema Serikali inaendelea kuzungumza na wadau ili kuangalia namna ya kutokomeza mazalia ya mbu wanaomsambaza ugonjwa huo, ikiwemo kutafuta fedha za kununua dawa za kuwa vijidudu hivyo.

Katika hatua nyingine, Ummy amesema taandika waraka wa kuhimiza usafi wa mazingira kwenye makazi ya wananchi kwenda Wizara ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI, ili viongozi wa Serikali za Mitaa wakasimamie zoezi hilo.

error: Content is protected !!