Tuesday , 26 September 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Miili ya waliofariki kwenye ajali ya treni India, kukabidhiwa baada ya vipimo vya DNA
Kimataifa

Miili ya waliofariki kwenye ajali ya treni India, kukabidhiwa baada ya vipimo vya DNA

Spread the love

 

TAKRIBANI watu 260 wamefariki na wengine karibu 650 wamejeruhiwa katika ajali ya treni iliyotokea nchini India, huku mamlaka zikisema, “waokoaji hawajaweza kuwapata watu wengine walionusurika kwenye ajali hiyo.” Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Ajali inayotajwa kuwa mbaya zaidi ya treni kuwahi kutokea katika karne hii, ilitokea usiku wa Ijumaa mashariki mwa jimbo la Odisha, imehusisha treni tatu zilizogangana. Mamia ya watu wengine wamejeruhiwa.

 Treni hizo, ni Coromandel Express iliyokuwa ikisafiri kutoka Howrah, jimbo la Bengali magharibi kuelekea Chenai, jimboni Tamil Nadu, na Howrah Superfast Express iliyokuwa ikisafiri kutoka Bengaluru huko Karnataka kuelekea Howrah.

Miili ya watu waliofariki dunia iliyofunikwa mashuka meupe ililazwa chini karibu na njia ya reli wakati wenyeji wa eneo ilikotokea ajali na waokoaji walipokuwa wakifanya juhudi kuwasaidia walionusurika.

Mkurugenzi wa kitengo cha dharura na zimamoto wa jimbo la Odisha, Sudhanshu Sarangi, alieleza kuwa kufikia majira ya saa nne usiku, walifanikiwa kuwaokoa watu walionusurika na baada ya hapo shughuli iliyofuata ilikuwa ya kuitoa miili ya watu waliokufa kwenye ajali hiyo.

Taarifa inaeleza kuwa takribani miili 280 ilipatikana Ijumaa usiku hadi Jumamosi asubuhi. Idadi ya majeruhi inatajwa kufikia watu 900 wakati uchunguzi wa chanzo hasa cha ajali hiyo ukiendelea. 


Kwa mujibu wa afisa mwandamizi wa India, P.K Jena, kati ya majeruhi hao, waliojeruhiwa vibaya ni 200 na wengine 200 waliruhusiwa kutoka hospitali baada ya kupatiwa matibabu. Raia wengi walijitokeza kutoa damu ili kuyanusuru maisha ya majeruhi.

Hata hivyo, Jena amesema wakati shughuli za uokoaji zikielekea ukingoni, moja ya changamoto kubwa ni kuitambua miili ya waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo.

Ameeleza kwamba ndugu wa marehemu watapatiwa miili ya ndugu zao pale watakapofanikiwa kuthibitisha kwa ushahidi uhusiano wao na baada ya miili kufanyiwa uchunguzi. Amesema, huenda vipimo vya vinasaba, DNA vikatumika ili kufanya utambuzi.

Waziri mkuu wa India, Narendra Modi, aliwasili katika eneo ilikotokea ajali hiyo huko Balasore Jumamosi na kuzungumza na waokoaji pamoja na kukagua uharibifu uliotokea. Alifika pia hospitali kuwajulia hali majeruhi.

Msemaji wa wizara ya reli, Amitabh Sharma amesema, mamlaka za reli zitaanza kuondoa mabaki ya treni zilizohusika kwenye kisa hicho ili kufanya matengenezo ya reli na kuruhusu kuendelea kwa safari za treni.

Awali, shughuli za uokoaji zilikwenda taratibu kutokana na treni mbili kuminyana. Maafisa wanasema, waokoaji 1,200 (elfu moa mia mbili), walifanya kazi na magari ya kubebea wagonjwa 115, mabasi 50 na vituo 45 vya afya vinavyohamishika usiku kucha.

Jana Jumamosi  ilitangazwa rasmi kuwa siku ya maombolezo kwenye jimbo la Odisha.

Licha ya juhudi za serikali za kuimarisha usalama wa reli, ajali nyingi za treni zimekuwa zikitokea kila mwaka katika taifa hilo lenye mtandao mkubwa zaidi wa reli duniani ulio chini ya usimamizi wa mamlaka moja.

Kwa mfano, Agosti 1995, treni mbili ziligongana karibu na mji mkuu New Delhi. Watu 358 walifariki dunia, katika moja kati ya ajali mbaya zaidi ya treni kuwahi kutokea nchini India.

Mwaka 2016, treni ya abiria iliteleza na kuacha njia yake katikati ya miji ya Indore na Patna ambao watu 146 walifariki.

Makosa ya kibinadamu na vifaa vya kutolea ishara vilivyopitwa na wakati ndivyo vinavyolaumiwa kusababisha ajali nyingi kati ya hizo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Uvamizi wa kijeshi Milango ya bahari ya Taiwan G7 yapinga China

Spread the loveMKUTANO wa Mawaziri wa Mambo ya nje wa nchi za...

Kimataifa

Rais Kagame kuwania muhula wa nne

Spread the loveRais wa Rwanda, Paul Kagame amesema atawania muhula wa nne...

Kimataifa

Ukraine kufungua kituo cha nafaka Kenya

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto amesema serikali ya Ukraine inapanga...

Kimataifa

Kufungwa kwa mpaka wa Tibet kulivyoathiri maisha ya Wanepali katika vijiji vya milimani

Spread the love  KALU Dhami kutoka Dhalain moja ya kata ya Manispaa...

error: Content is protected !!