August 13, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Miili City Boys yatambuliwa, maiti waongezeka

Spread the love

WATU waliofariki dunia kwenye ajali ya Basi la City Boys iliyotokea jana katika Kijiji cha Maweni, Singida wameongezeka na kufikia 30 huku baadhi ya miili ikitambuliwa, anaandika Dany Tibason.

Kati ya miili 31, watu 13 tayari wametambuliwa. Maiti hao walikuwa wamehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari mjini humo, Ibenzi Ernest, daktari wa ajali na mifupa amesema, hospitali hiyo jana ilipokea maiti 27 na kwamba. Leo mtu mwingine amefariki dunia.

Dk. Ernest amesema jana jumla ya maiti zilizofikishwa katika hospitali ya Rufaa mkoani hapa zilikuwa 27 ambapo maiti moja imeongezeka baada ya kufariki majira ya saa tano asubuhi na kufanya idadi ya maiti kuwa 28.

Dk. Ernest amewataja maiti walitambuliwa kuwa ni John Lukanda, Ismail Bashe, Paul Mfaume, Deogratius Wajibiri, Rabia Lema, Levoso Israel, Leonard Nyamatokela, Jesca Lazaro, Betty Acent, Paulina Mheza, Restar Exavery na Kefuni Deus.

Pamoja na kuwa maiti zimetambuliwa Dk. Ernest amesema, majeruhi waliofikishwa hospitalini hapo ni 15, kati ya hao mmoja amefariki na mmoja amelazwa katika chumba cha magonjwa mahututi.

Thobias Sedoyeka, Kamanda wa Polisi Mkoa Singida amesema, waliofia katika Hospitali ya Manyoni ni watatu na kufikisha idadi ya maiti kuwa 31.

Kwa Mujibu wa Kamanda Sedoyeka, dereva wa basi la City Boys lililokuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Kahama, Jeremiah Martini (34) Mkazi wa Dar es Salaam anashikiliwa na jeshi hilo ambapo dereva wa basi la kampuni hiyo hiyo lililokuwa likitoka Kahama kwenda Dar es Salaam alifariki katika ajali hiyo.

error: Content is protected !!