
Mchimbaji madini wa Mererani akiwa kazini
Zaidi ya migodi 15 ya machimbo ya madini ya Tanzanite katika Kitalu B-Mererani, Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara, imeteketea kwa moto unaodhaniwa kusababishwa na hitirafu ya umeme.
Taarifa za awali, zinasema kuwa pamoja na kwamba hakuna mtu aliyedhurika lakini mali zote zikiwemo mashine za uchimbaji na vibanda vya kazi ya wachimbaji zimeteketea.
Kutokana na ajali hiyo ya moto, wachimbaji zaidi ya 1500 wamepoteza ajira zao huku baadhi ya wamiliki wa migodi hiyo wakilichukulia tukio hilo kama hujuma dhidi yao.
More Stories
Jamhuri yakwamisha kesi ya Chadema dhidi ya Jeshi la Polisi
Sh54 Bil. kugharamia mradi wa maji Chiuwe
Serikali yapewa neno ununuzi treni zilizotumika