Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko ‘Mifupa ya binadamu yazagaa Mwanza’
Habari Mchanganyiko

‘Mifupa ya binadamu yazagaa Mwanza’

Angelina Mabula, Mbunge wa Jimbo la Ilemela
Spread the love

ANGELINA Mabula, NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi, ameitaka halmashauri ya Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela, kuhakikisha zinamaliza uhaba wa maeneo ya makaburi ili kutatua tatizo la mifupa ya binadamu inayozagaa kwenye makaburi jijini hapa, anaandika Moses Mseti.

Maeneo ya makaburi ambayo yanatajwa kuwa na mifupa ya binadamu na kuibua hofu kwa wananchi ni pamoja na makaburi ya Kitangiri (Ilemela) na Igoma (Nyamagana).

Pia imegundulika kwamba asilimia 95 ya migogoro ya ardhi iliyopo jiji la Mwanza inahusu madai ya fidia ambapo zinahitajika zaidi ya Sh. bilioni nane kumaliza hali hiyo, inayohusisha maeneo yaliotengwa kwa ajili makaburi.

Mwanasiasa huyo alizungumza na watumishi wa Jiji la Mwanza idara ya ardhi na kutembelea maeneo mbalimbali ya Ilemela na Nyamagana na kupokea taarifa za urasimishaji makazi na ulipaji kodi za majengo.

Mabula amesema kuwa Jiji la Mwanza lina changamoto kubwa ikiwamo uhaba wa makaburi kutokana na maeneo mengi yaliyotengwa katika kipindi cha nyuma kujaa huku Jiji hilo likikosa uwezo wa kulipa fidia katika maeneo yaliyotengwa na ili kuhamisha wananchi.

Amesema kwamba kwa sasa asilimia 95 ya migogoro inahusu fidia na kwamba zinahitajika zaidi ya Sh bilioni nane ili kumaliza tatizo hilo.

“Haiwezekani mkashindwa kuwasitiri wenzenu walioitwa na Mungu, naomba hakikisheni mnapopima aradhi wekeni maeneo ya makaburi na mlipe fidia, tunakoelekea ni kuleta ugomvi makaburini maana itafikia mahala ndugu watazuia kaburi la mtu wao lisifukuliwe, chukueni hatua haraka,”amesema Mabula.

Mabula ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilemela, amesema katika wilaya yake hususan katika makaburi ya Kitangiri, mifupa ya binadamu imekuwa ikizagaa hivyo, kitendo ambacho aliomba Halmashauri hizo kuangalia namna bora ya kutatua tatizo hilo.

Katika hatua nyingine, Mabula aligusia mgogoro wa Luchelele uliodumu kwa miaka zaidi ya mitano huku akilitaka Jiji la Mwanza kuacha kuwaondoa kwenye maeneo yao, ambao walikuwa na wakilalamikia kwa muda mrefu na kuomba yaendelezwe kulingana na michoro.

Pia Mabula aliagiza uongozi wa Jiji kutafuta eneo lingine na kulipatia Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ili kujenga nyumba za watumishi wa Serikali na zile za kuwauzia watu binafsi kama ilivyofanyika katika Wilaya kata ya Buswelu Wilaya Ilemela.

Benedict Kilimba, Meneja wa NHC Mkoa wa Mwanza, alisema kuwa tatizo la upatikanaji wa eneo la kujenga mji wa makazi bora ya kisasa yamekuwa ni kero kubwa kwake na yanayomnyima usingizi usiku na mchana na kuuomba uongozi wa jiji hilo kuitafutia shirika maeneo yasiokuwa na mgogoro.

Naibu waziri huyo, yupo mkoani Mwanza kwa ziara ya kikazi ya siku tano kutembelea wilaya zote za mkoa huo ili kupokea taarifa mbalimbali na kukagua shughuli za miradi iliyopo chini ya wizara hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!