June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Michezo mashuleni yahimizwa

Spread the love

AFISA Elimu wa Mkoa wa Dodoma, Juma Kaponda amewataka maafisa michezo kuhakikisha timu zao zinafanya vizuri katika mashindano ya Umoja wa Shule za Msingi (Umitashumta) na ule wa Sekondari (Umiseta). Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Hayo ameyasema leo katika kikao cha kazi cha watendaji wa sekta ya elimu na ngazi ya halmashauri ya mkoa.

Kaponda amesema maafisa elimu wanatakiwa kuwa na timu za mfano ili pindi yanapotokea mashindano wasipate tabu ya kutafuta wachezaji.

“Nataka maandalizi kwa ajili ya mashindano ya Umitashumta na Umiseta yaanze sasa na nataka hili lizingatiwe kwanza maafisa michezo wawe na timu za mifano,’’ amesema.

Kaponda amesema pia ni lazima kila wilaya iweke mkazo kwenye michezo ambayo haipewi nafasi ya kuchezwa na vijana wengi.

“Kuna michezo ni lazima tuitafutie walimu na nyie maafisa michezo sio mnajiita watu wa michezo wakati hamjui kitu waachieni wale wenye taaluma waifanye kazi hiyo,’’ amesema.

error: Content is protected !!