July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Miche 35,000 yapandwa Dodoma

Spread the love

ZAIDI ya miche 35,000 ya miti mbalimbali imepandwa wilayani Chamwino, Dodoma ikiwa ni pamoja na mahali ilipo Ikulu ndogo ya rais katika Kijiji cha Chamwino, anaandika Dany Tibason.

Hatua hiyo imeelezwa kuwa ni jitihada za kuunga mkono zoezi la upandaji miti kitaifa lenye lengo la kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na ukame.

Akizungumza na wananchi walioshiriki zoezi la upandaji miti leo Farida Mgomi, Mkuu wa Wilaya hiyo amewataka wananchi hao kuwa mfano wa kuigwa katika maeneo yao.

Aidha katika hatua nyingine serikali wilayani humo imewataka wananchi kuhakikisha kuwa zoezi hilo linakuwa endelevu na kuacha tabia ya kukata mti bila kupanda.

Katika kuhakikisha mazingira yanatunzwa eneo hilo, mti uliopandwa mwaka 1984 na Baba wa taifa, Mwalimu Julius Nyerere bado unaonekana kuwa imara.

error: Content is protected !!