August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Michango ya Mwenge yatinga bungeni

Askari wakiulinda Mwege wa Uhuru

Spread the love

MBUNGE wa Viti Maalum, Rhoda Kunchela (Chadema) ameomba mwongozo wa kutaka Mwenyekiti wa Bunge Andrew Chenge kuharisha shughuli za bunge kwa lengo la kujadili adha ya watumishi, wafanyabiashara na walimu kuchangishwa fedha za Mwenge, anaandika Dany Tibason.

Mbunge huyo amesema kuwa licha ya kuwa michango ni hiari lakini serikali imekuwa ikiwalazimisha wafanyabiashara, watumishi wa Umma na walimu kulipa michango ya Mwenge kwa lazima.

Amesema kutokana na hali hiyo serikali inatakiwa ieleze ni kwanini michango ya Mwenge imekuwa ikichangishwa kwa lazima wakati kila mmoja anatakiwa kuchanga kwa hiari yake.

Katika kuelezea kuwepo kwa michango hiyo amesema anazo risiti nyingi ambazo watumishi pamoja na wafanyabiashara wanazopewa kwa kuchangishwa michango hiyo kwa lazima.

“Mheshimiwa mwenyekiti naomba kiti chako kiweze kutoa ufafanuzi wa jambo hili kila mtu anajua kuwa michango ni hiari ya mtu lakini kumezuka tabia ya halmashauri kuwachangisha watumishi, wafanyabiashara na walimu kuchangishwa kwa lazima.

“Kwa kuwa jambo hili linaonekana kuwa tatizo kubwa katika jamii imekuwa ikikubwa na wavitisho pale ambapo wanachelewa kuchangia shughuli mbalimbali hususani mbio za Mwenge,” amesema Kunchela.

Akijibu hoja ya mbunge huyo, Chenge amesema pamoja na kuwa mbunge huyo katoa hoja hiyo bungeni lakini bado haikupaswa kuzungumziwa bungeni.

Hata hivyo amemtaka mbunge huyo kuwasilisha risiti za malipo mezani kwa kiti cha spika ili ziwasilishwe serikalini ili kuona ni jinsi gani ya kutafuta mfumbuzi wa jambo hilo.

error: Content is protected !!