Sunday , 29 January 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Miaka 60 ya Uhuru: THRDC yasema hili kosa tulirekebishe
Habari Mchanganyiko

Miaka 60 ya Uhuru: THRDC yasema hili kosa tulirekebishe

Mratibu wa THRDC, Onesmo Olengurumwa
Spread the love

 

WAKATI Tanzania Bara kesho Alhamisi, tarehe 9 Desemba 2021, inatimiza miaka 60 ya Uhuru, Watanzania wametakiwa kutorudia kosa la kuwaachia viongozi jukumu la kuamua maendeleo yao. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Wito huo umetolewa leo Jumatano, tarehe 8 Desemba 2021, Dar es Salaam, katika mdahalo wa kitaifa juu ya hali ya haki binadamu nchini katika kipindi cha miaka 60, ulioandaliwa na wizara ya katiba na sheria, kwa kushirikiana na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC).

Mratibu wa THRDC, Onesmo Olengurumwa, amesema ili Tanzania iwe na maendeleo, inatakiwa wananchi washiriki kikamilifu kwenye mipango ya maendeleo, badala ya kuwaachia jukumu hilo viongozi pekee.

“Taifa lolote mnaloliona lina maendeleo duniani, ni lile wananchi wanakuwa sehemu ya kuleta maendeleo, wanakuwa sehemu ya mipango lakini na kufanya tathimini ya kuangalia kama taifa wanakwenda wapi, wanatoka wapi na changamoto ni zipi,” amesema Olengurumwa na kuongeza:

“Nadhani hili kosa tulirekebishe, tunapofanya tahimini ya miaka 60 nadhani tusiwaachie viongozi wetu wenyewe wawe wanakaa wanakutana na kufanya tathimini.

Akizungumza katika madahalo huo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Amon Mpanju, amesema jukumu la kuleta maendeleo na kulinda haki za binadamu, sio la Serikali peke yake, bali ni la Watanzania wote.

“Sababu suala la haki za binadamu sio ya Serikali tu, ni letu sote, tutafakari namna gani sisi sote tutahimiza kwa mawanda yake namna gani kila mmoja wetu ametimiza wajibu wake kukuza na kuendeleza haki za binadamu nchini,” amesema Mpanju.

Mpanju amewataka wadau walioshiriki mdahalo huo, kutumia fursa hiyo kujadili kwa kina masuala ya haki za binadamu, ikiwemo kuibua changamoto zake ili Serikali izitafutie ufumbuzi.

“Tathimini ya leo isilenge kuangalia kwenye elimu, hapana tunafanya tathimini ya masuala ya haki za binadamu tangu tupate elimu, haki za binadamu zimejumuisha haki za kisiasa, kiraia, kijamii na haki za kiutamaduni,” amesema Mpanju na kuongeza:

“Unapoongelea haki za binadamu unaongelea nguzo kuu ya binadamu ya utu, huwezi ongelea maendeleo ya miundombinu, sayansi na teknolojia bila kuwa na haki za binadamu, miundombinu ni nyenzo za kutuwezesha sisi kuzifurahia na kuzifikia haki za binadamu.”

Mdahalko huo kwa sasa unaendelea ambapo watu mbalimbali mashuhuri wanashiriki, akiwemo Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, aliyekuwa Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu nchini (LHRC), Dk. Helen Kijo-Bisima, pamoja na mabalozi kutoka nchi mbalimbali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Huawei Tanzania yatajwa miongoni mwa waajiri bora kimataifa

Spread the loveKAMPUNI ya Huawei Tanzania imetajwa kuwa mwajiri bora nchini na...

Habari Mchanganyiko

Waziri wa uchumi wa Finland atua nchini, kuteta na mawaziri 7

Spread the loveWAZIRI wa Masuala ya Uchumi wa Finland, Mika Tapani Lintilä...

Habari Mchanganyiko

Asimilia 79 wafeli somo la hesabu matokeo kidato cha nne

Spread the loveWATAHINIWA wa shule 415,844 sawa na asilimia 79.92 ya watahiniwa...

Habari Mchanganyiko

NECTA yafuta matokeo ya watahiniwa 333 kwa kuandika matusi, kudanganya, 286 yazuiwa

Spread the loveBARAZA la Mitihani la Tanzania (Necta) leo Jumapili limetangaza kuyafuta...

error: Content is protected !!