October 23, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Miaka 51 ya Muungano, Lamudi yahimiza uwekezaji

Marais wa Tanganyika na Zanzibar, Julius Nyerere (kushoto) na Aman Abeid Karume wakisaini hati ya Muungano

Spread the love

KAMPUNI ya Lamudi Tanzania imeungana na Watanzania wote kusherekea miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, huku ikihamasisha wawekezaji kutoka ndani na nje kuwekeza visiwani Zanzibar.

Mkurugenzi Mtendaji wa Lamudi Tanzania, Mustafa Suleimanji ameliambia MwanaHALISI Online, kuwa Watanzania wanatakiwa kujivunia Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwani ndiyo kitovu cha amani ya nchi ya Tanzania.

Suleimanji alisema kutokana na amani iliyopo inawashawishi wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuwekeza kwa wingi katika sekta ya mali zisizohamishika kama majengo ya makazi na biashara.

“Tanzania na Zanzibar ni miongoni mwa nchi zilizoungana kwa muda mrefu huku badoi zikiwa na amani na demokrasia, hii inatoa fulsa kwa wawekezaji kuwekeza. Lamudi tunapenda kuwahamasisha kuwekeza katika nchi hizo ili kuinua uchumi na mapato,” anasema Mustafa Suleimanji.

Naye Meneja Mkuu wa Lamudi Tanzania, Godlove Nyagawa anasema pamoja na kuwepo kwa wawekezaji wengi wanaowekeza kwenye sekta ya mali zisizohamishika kama majengo, lakini uwezekaji huo upo kwenye baadhi ya majiji ya Tanzania Bara.

Nyagawa amesema wawekezaji sasa wanatakiwa kupanua miradi yao hadi Zanzibar pamoja na mikoa mingine iliyokuwa Tanzania Bara kama Dodoma, Singida, Mtwara, Iringa ili iwe na miradi mikubwa kama ilivyokuwa jijini Dar es Salaam na majiji mengine.

Tangu mwaka 1964 mpaka mwaka huu 2015, Tanzania imekuwa kwa kasi katika uchumi, siasa, kijamii, hivyo Lamudi Tanzania inatabiri kuwa kutakuwa na ukuaji mkubwa wa sekta ya mali zisizohamishika.

Aprili 26, 1964, Tanganyika na visiwa vya Zanzibar ziliungana na kuunda Jamhuri ya Muungano ya Tanzania. Jina la taifa jipya lilitokana na Muungano wa nchi hizo ambapo Tan ilitokana na jina la Tanganyika na Zan ilitoka kwenye jina la Zanzibar na Nia ilitokana na nia yao ya kuungana.

error: Content is protected !!