May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Miaka 44 ya CCM: Dk. Bashiru ‘hatujapotea’

Dk. Bashiru Ally, Katibu Mkuu wa CCM

Spread the love

DAKTARI Bashiru Ally, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ametetea chama chake kwamba hakijapetea katika misingi ya demokrasia. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Amesema, licha ya mabadiliko ya mfumo na muundo uliyofanyika katika chama chake, utaifa na demokrasia vimezingatiwa.

Dk. Bashiru ametoa kauli hiyo leo tarehe 6 Februari 2021 wakati akitaja sifa za CCM katika Maadhimisho ya Miaka 44 ya chama hicho, yaliyofanyika jijini Dodoma. Katibu Mkuu huyo wa CCM, amesema chama hicho ni cha mabadiliko na kwamba kimefanya mabadiliko makubwa katika sera zake, muundo na mifumo.

“Sifa ya tatu ni chama cha mabadiliko, ndio maana kinaitwa cha mapinduzi, hatua kwa hatua tumefanya mabadiliko makubwa sana, hata katika sera zetu, miundo ya chama chetu na mifumo yetu, lakini hatujapoteza misingi ya utaifa, demokrasia na mabadiliko,” amesema Dk. Bashiru.

Akielezea sifa za CCM, Dk. Bashiru amesema, ziko tatu ambazo ni chama cha kidemokrasia, chama chenye wanachama wengi na ya mwisho ni chama cha mabadiliko.

“Chama chetu kina sifa kubwa tatu, ambazo zinakipambanua na vyama vingine vya siasa ndani na nje ya nchi yetu, sifa ya kwanza ni chama cha kitaifa. Chama pekee Afrika ambacho kina wanachama wa aina zote, wenye sura ya Taifa zima,” amesema Dk. Bashiru.

Dk. Bashiru amesema “sifa ya pili ni chama cha kidemokrasia, hilo sitaki kupoteza muda kulizungumzia.”

error: Content is protected !!