December 8, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Miaka 19 ya Mv Bukoba, Sumatra yaonywa

Wananchi wa Mwanza wakiwa kaytika makabuli waliyozikwa abiria waliofariki kwenye meli ya MV Bukoba

Spread the love

MKUU wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo, ameitaka Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra), kuhakikisha inafanya ukaguzi wa mara kwa mara katika Ziwa Victoria ili kudhibiti ajali zisizo za lazima. Anaandika Moses Mseti, Mwanza … (endelea).

Kauli hiyo ameitoa leo, wakati wa kumbukumbu ya ajali ya meli ya Mv Bukoba iliyotokea Mei 21,1996 na kusababisha vifo vya watu wengi; iliyofanyika katika makaburi ya pamoja yaliyopo kata ya Igoma wilayani Nyamagana.

Mulongo ambaye aliwakilishwa na Katibu Tawala wa llemela, Rahima Bakari, amesema endapo mamlaka hiyo itafanya ukaguzi wa mara kwa mara, tatizo la ajali litapungua na kulinda usalama wa Watanzania ambao wanatumia usafiri wa majini.

Pia, amesema upakiaji wa abiria na mizigo kupita kiasi, kunaweza kusababisha ajali zisizo za lazima, hivyo ni bora wafanyabiashara, watumiaji wa usafiri huo kuhakikisha wanafuata kanuni na taratibu za usafiri kama zinavyoelekeza.

Mwanamitindo wa kimataifa ambaye alimpoteza mama yake katika ajali hiyo, Fulaviana Matata, amesema tukio hilo ni kati ya matukio ambayo hayatasahaulika kwenye maisha yake kutokana na kumpoteza mzazi wake akiwa na umri mdogo.

“Tukio hili, siwezi kulisahau katika maisha yangu, ndio maana siwezi kulizungumzia. Nashukru wote ambao wameacha shughuli zao kuja kujumuika wote,” amesema Matata.

Mpaka sasa imetimia miaka 19 tangu kutokea kwa ajili hiyo, iliyopoteza maisha ya watu 800 na mali nyingi kupotea.

error: Content is protected !!