Tuesday , 16 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Mhuhiri Mackenzie, mkewe walalamika polisi kuwanyima chakula
Kimataifa

Mhuhiri Mackenzie, mkewe walalamika polisi kuwanyima chakula

Spread the love

MHUBIRI mwenye utata kutoka nchini Kenya, Paul Mackenzie pamoja na mkewe ambao wamedaiwa kusababisha vifo vya zaidi ya watu 100 ambao waliwalazimisha kufunga ili kukutana na Yesu, wamelalamika kuteswa wakiwa mahabusu na kunyimwa chakula. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

Mawakili wa Mackenzie, Elisha Komora na George Kariuki wamekanusha madai yaliyotolewa na upande wa mashtaka kwamba wateja wake walikuwa wakitunzwa vyema na polisi wakiwa korokoroni.

Wakati wa kusikizwa kwa kesi dhidi yake katika Mahakama ya Shanzu jana Ijumaa, Komora aliiarifu mahakama kwamba kwa siku mbili tangu waondoke mahakamani Jumanne tarehe 2 Mei 2023 hawajala.

Wakili huyo pia alisema kabla ya mteja wake kuletwa mahakamani, maafisa wa polisi waliwanyima kiamsha kinywa.

“Madai ya serikali kwamba washukiwa wazidi kushikiliwa ilhali wanakosa mlo ni ya kupotosha. Asubuhi ya leo wateja wangu hajapata kifungua  kinywa. Washtakiwa walinyimwa chakula kwa siku mbili tangu waondoke mahakamani  ” Komora alisema. Komora pia alisema kwamba Mackenzie na mtuhumiwa mwenza walikuwa wakipokea kichapo kutoka kwa maafisa wa polisi wakiwa mahabusu.

“Washtakiwa pia walipigwa wakiwa ndani ya selo. Kwa serikali kusema wanatunzwa vyema wakati wakizuiliwa sio kweli,” wakili huyo aliongeza.

Pia alidai kwamba mkewe Mackenzie, Rhoda Mumbua Maweu, ambaye alitiwa mbaroni akiwa na bintiye wa miaka miwili na nusu, hawakupewa chakula. Alisema walilazimika kununua chakula na maji kwa ajili ua mtoto huyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

Habari za SiasaKimataifa

Rais Faye amteua aliyekuwa mfungwa mwenzie kuwa waziri mkuu

Spread the loveRais mpya wa Senegal, Bassirou Diomaye Faye, amemteua Ousmane Sonko...

error: Content is protected !!