Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Mhasibu wa halmashauri, msaidizi jela miaka saba kwa wizi Mil 34
Habari Mchanganyiko

Mhasibu wa halmashauri, msaidizi jela miaka saba kwa wizi Mil 34

Spread the love

MAHAKAMA ya Wilaya ya Simanjiro Mkoa wa Manyara nchini Tanzania imemhukumu Peter Mollel, aliyekuwa Mhasibu wa Halmashauri ya Simanjiro kifungo cha miaka saba gerezani kwa makossa ya wizi akiwa mtumishi wa umma. Anaripoti Mwandishi Wetu, Manyara … (endelea).

Pamoja na adhabu hiyo iliyotokana na makossa 11 ya wizi yaliyofanywa na Mollel, ametakiwa kulipa faini ya Shilingi 4 milioni kwa kila kosa katika makossa tisa ya matumizi ya nyaraka kumdanganya mwajiri sawa na Shilingi 36 milioni au kifungo cha miaka mitatu jela.

Taarifa iliyotolewa leo Ijumaa tarehe 8 Mei 2020 na Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Manyara, Holle Makungu imesema hukumu hiyo ya kesi ya jinai namba CC.48/2016 ilitolewa jana Alhamisi tarehe 7 Mei 2020 na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Arusha, John Mkwabi.

Katika hukumu hiyo, Mkwabi alimhukumu Mollel kifungo cha mwaka mmoja gerezani bila faini kwa makossa mawili ya matumizi mabaya ya madaraka kinyume cha K/F cha 31 cha Sheria ya Kuzia na Kupambana na Rushwa namba 11/2007.

Mwingine aliyetiwa hatiani katika kesi hiyo na kupewa adhabu sawasawa na Mollel ni mhasibu msaidizi katika halmashauri hiyo, Ester Melkior ambao kwa pamoja walipelekwa gerezani kuanza kutumikia kifungo.

Awali, waendesha mashtaka wa Takukuru, Isdory Kyando akisaidiwa na Adamu Kilongozi waliwafikisha washtakiwa hao mahakamani hapo na kuwasomea jumla ya makossa 24, katika makossa hayo, 10 yalihusu kutumia nyaraka za kumdanganya mwajiri.

Makossa mawili yalihusu matumizi mabaya ya madaraka, makosa 12 yalihusu wizi uliofanywa na washtakiwa wakiwa watumishi wa umma kinyume na vifungu vya 258 na 270 vya sheria ya kanuni ya adhabu.

Waendesha mashtaka hao waliwasilisha ushahidi usioacha shaka mahakamani hapo kuonyesha kwamba, kati ya mwaka 2008 na 2010 mshtakiwa wa kwanza kwa nafasi yake ya mweka hazina wa halmashauri alikuwa ndiye muidhinishaji wa nyaraka hizo na mshtakiwa wa pili kwa nafasi yake ya mhasibu msaidizi ndiye aliyeandaa nyaraka hizo.

Kwa pamoja walishirikiana kuzidisha orodha ya walipwaji na kiasi cha mishahara ambacho walipaswa kulipwa kwenye hati za malipo, kisha kuziwasilisha nyaraka hizo benki kwa ajili ya malipo.

Fedha hizo zilizozidi zilikuwa zinaingizwa kwenye akaunti za benki za washtakiwa na kisha washtakiwa hao kuzitumia kwa manufaa yao.

Jumla ya fedha hizo walizojipatia kutokana na udanganyifu huo ni Shilingi 34.52 milioni.

Kabla ya adhabu hiyo kutolewa na Mkwabi, wakili wa utetezi Justus Ilyarugo aliiomba mahakama iwapunguzie adhabu washtakiwa kwa kuwa mshtakiwa Mollel ni baba mwenye familia inayomtegemea.

Wakili Ilyarungo aliiomba pia mahakama imuonee huruma na kumpunguzia adhabu mshtakiwa wa pili, Ester kwa kuwa ni mama mwenye mtoto mmoja, hana mme na pia ni mlezi wa mama yake mzazi.

Kwa upande wa waendesha mashtaka wa Takukuru, Kyando na Kilongozi waliiomba Mahakama itoe adhabu kali kwa washtakiwa kwa kuwa makossa waliyotenda ya rushwa na wizi, wakiwa watumishi wa umma ni kati ya makossa mabaya na ndiyo maana Bunge la Tanzania liliweka adhabu kali kwa makossa hayo ili iwe fundisho kwa watumishi wa umma wenye fikira za wizi na rushwa katika utumishi wa umma.

Baada ya kusikiliza na kuzingatia hoja zilizotolewa na upande wa mashtaka na upande wa utetezi, Mkwabi alitoa addhabu hiyo kwa mujibu wa sheria kulingana na makosa ambayo washtakiwa waliyatenda.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!