January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mhariri wa MwanaHALISI, Kamukara kuagwa kesho Leaders

Mwandishi Edson Kamukara enzi za uhai wake

Spread the love

MHARIRI mwanzilishi wa gazeti la hili, Edson Kamukara, anatarajia kuagwa kesho kwenye viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es Salaam kuanzia saa nne asubuhi.

Marehemu Kamukara ambaye alifariki dunia nyumbani kwake Mabibo jijini Dar es Salaam, jana jioni, na msiba uko nyumbani kwa dada yake Makongo Juu, jirani na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT).

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na kampuni aliyokuwa anafanya kazi marehemu Kamukara, Hali Halisi Publishers Limited (HHPL), wachapishaji wa magazeti ya MwanaHALISI, MSETO, MwanaHALISI ONLINE na mtandao wa MwanaHALISI Forum, mwili wa marehemu utawasili viwanjani hapo saa nne asubuhi.

Meneja wa HHPL, Robert Katula amesema kuwa baada ya mwili kuwasili uwanjani kutakuwa na misa ya kumuombea marehemu na baada ya hapo utaratibu wa kutoa heshima ya mwisho kwa marehemu zitaanza kabla ya kuanza kwa safari ya kusafilisha mwili nyumbani kwao, Muleba Kusini kwa mazishi.

Katula amesema taratibu za mazishi za nyumbani kwao zitafanyika baada ya mwili wa marahemu kuwasili nyumbani kwao Muleba ya Kusini.

MwanaHALISI Online itaendelea kuwapa taarifa yakinachoendela katika msiba huo 

Mwandishi Edson Kamukara enzi za uhai wake
Mwandishi Edson Kamukara enzi za uhai wake

BWANA AMETOA, BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE, AMINA 

error: Content is protected !!