Friday , 3 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Mhandisi Mfugale kuzikwa Julai 5 Iringa
Habari Mchanganyiko

Mhandisi Mfugale kuzikwa Julai 5 Iringa

Aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Mhandisi Patrick Mfugale
Spread the love

 

MWILI wa aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Mhandisi Patrick Mfugale, unatarajiwa kuzikwa Jumatatu ya tarehe 5 Julai 2021, nyumbani kwao Ifunda mkoani Iringa. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Mhandisi Mfugale alifariki dunia tarehe 29 Juni 2021, katika Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma, alikokuwa anapatiwa matibabu baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Kwa mujibu wa ratiba ya mazishi ya Mhandisi Mfugale, shughuli za kuuaga mwili wake zitaanza kesho tarehe 1 Julai mwaka huu, jijini Dodoma na kwamba viongozi mbalimbali kutoka Serikalini watatoa heshima zao za mwisho.

Baada ya mwili huo kuagwa jijini Dodoma, utasafirishwa kuelekea mkoani Dar es Salaam, ambapo utalazwa katika Hospitali ya Lugalo, kisha Ijumaa tarehe 2 Julai 2021, utapelekwa katika Viwanja vya Karimjee kwa ajili ya kuagwa.

Ratiba hiyo imesema, mwili huo baada ya kuagwa katika viwanja hivyo, utapelekwa nyumbani kwa marehemu Mhandisi Mfugale, maeneo ya Kimara Temboni.

Jumamosi ya tarehe 3 Julai 2021, mwili huo utasafirishwa kuelekea Ifunda na kuwasili Jumapili ya tarehe 4 Julai mwaka huu.

Ibada ya kutoa heshima za mwisho itafanyika Jumatatu tarehe 5 Julai 2021, baadae shughuli za mazishi zitafanyika kuanzia saa tisa alasiri hadi saa 11:00 jioni.

Mhandisi Mfugale alizaliwa 1950 mkoani Iringa, alipata elimu ya Sekondari katika Shule ya Moshi 1975. Mhandisi huyo alipata Shahada ya Kwanza ya Uhandisi 1983, katika Chuo Kikuu cha Roorkee nchini India.

1995 alipata Shahada ya Pili kwenye Chuo Kikuu cha Loughborough nchini Uingereza.

2003 alipokea tuzo ya Bodi ya Wahandisi Tanzania. 2018 alipokea tuzo ya utekelezaji uhandisi.

Mhandisi Mfugale atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika ujenzi wa miundombinu nchini, aliwahi kutengeneza mfumo wa usimamizi madaraja (Bridge Management System).

Enzi za uhai wake, alisimamia ujenzi wa madaraja zaidi ya 1,400, ikiwemo daraja la Mkapa Rufiji, Daraja la Umoja linalounganisha Tanzania na Msumbiji lililoko mkoani Ruvuma na Daraja la Rusumo mkoani Mara.

Mengine ni, Daraja la Kikwete lililoko mto Maragarasi mkoani Kigoma na Daraja la Juu la Tazara ambalo limepewa jina lake la Mfugale Flyover.

Pia, alisimamia ujenzi wa Daraja la Juu la Ubungo linaloitwa Daraja la Kijazi pamoja na Daraja la Tanzanite linaloendelea kujengwa Dar es Salaam na Daraja la John Pombe Magufuli, linalounganisha Kigongo hadi Busisi mkoani Mwanza.

Mhandisi Mfugale aliajiriwa katika Wizara ya Ujenzi 1977, aliteuliwa kuwa Mtendaji Mkuu wa Tanroads tarehe 23 Mei 2011 na Magufuli, wakati huo alikuwa Waziri wa Ujenzi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Ndege ya Precision Air yaahirisha safari kwa hitilafu, nyingine yatua kwa dharura

Spread the love  NDEGE ya Shirika la Precision Air imeshindwa kufanya safari...

Habari Mchanganyiko

NMB yakabidhi vifaa tiba hospitali Mtwara  

Spread the loveBENKI ya NMB Kanda ya Kusini imetoa msaada wa vifaa...

Habari Mchanganyiko

Kasilda Mgeni anasisitiza umoja, ushirikiano Same 

Spread the love  MKUU mpya wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda...

Habari MchanganyikoTangulizi

Hii hapa kauli ya Sheikh mpya mkoa wa Dar

Spread the loveSAA chache baada ya kuteuliwa kukaimu nafasi ya aliyekuwa Sheikh...

error: Content is protected !!