April 12, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mhagama akumbusha uzalendo watumishi wa Mashirika ya Kimataifa

Jenista Mhagama, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu)

Spread the love

JENISTA Mhagama, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) ametoa wito kwa Watanzania wanaofanya kazi katika Mashirika ya Kimataifa kuitumia fursa hiyo katika kusukuma gurudumu la maendeleo ya taifa lao. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Mhagama ametoa wito huo leo tarehe 15 Juni 2019 wakati akizungumza katika Kongamano la Nne la Tafa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lililofanyika Jijini Dodoma.

Akitolea mfano wa Amon Manyama, Mkuu wa Programu wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa nchini (UNDP), Mhagama amesema ni vyema Watanzania hao wakaiga mfano wake katika kutumia mashirika yao kuchochea ustawi wa Watanzania.

“Tunayo mashirika mbalimbali ya kimataifa yanayofanyakazi ndani ya taifa letu, na Watanzania wamepata fursa ya kutumikia mataifa hayo. Lakini kazi anayofanya Manyama kama muwakilishi kwa ustawi wa Watanzania ni kubwa sana,” amesema Mhagama na kuongeza:

“Labda tu nichomekee hapo, Watanzania wengine ambao wako katika mashirika mbalimbali ya kimataifa watusaidie kama kazi anayofanya ndugu yangu Manyama. Sisemi kama hawafanyi ila watufikishe kama anavyofanya Manyama.”

error: Content is protected !!