JUTORAM Kabatele Mahala, ni Mtanzania aliyebuni alama sita za barabarani kwa ajili ya kuwalinda makundi ya watu wenye walemavu barabarani ambazo zinatumika kwa miaka kadhaa sasa. Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam…(endelea).
Kabatele ni Baba wa familia ya mke mmoja na watoto wanne na licha ya mchango wake huo kwa taifa kutambulika na watu wachache, bado hajanufaika wala taifa halijatambua mchango wake kama muanzilishi wa kutumika kwa alama hizo.
Kwa sasa anaishi Vingunguti jijini Dar es Salaam ambapo Serikali ya mtaa ilimpa jina la mtaa huko anapoishi.
Mtaa huo unaoitwa Kabetele Street uliopo katika eneo la Mtambani, pia aliwahi kupata tuzo za mbunifu bora wa alama za barabarani kwa watu wenye ulemavu mwaka 2019 kupitia tuzo za ‘I Can Award’ aliyotunukiwa na marehemu, aliyekuwa Mwenyekiti wa Kampuni za IPP, Reginald Mengi.
Lakini licha ya hayo yote, bado anataabika kwa ufukara huku alama zake zinatumika kwenye vitabu mbalimbali vya mafunzo ya usalama barabarani vyuoni na serikalini huku akimwomba Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli amsaidie.
Fuatilia mahojiano yake na MwanaHALISI TV .
Leave a comment