August 15, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mgunda atoa tahadhari kwa Mayele kesho

Juma Mgunda

Spread the love

 

KOCHA Mkuu wa kikosi cha Coastal Union ya Tanga, Juma Mgunda amesema kwenye mchezo wa kesho wa fainali dhidi ya Yanga, hawatocheza na mshambuliaji hatari Fiston Mayele bali watadili na timu nzima. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Arusha … (endelea)

Mchezo huo wa fainali utapigwa kesho kwenye dimba la Sheikh Amri Abeid jijini Arusha majira ya saa 9:30 jioni.

Wakati akiongea na waandishi wa Habari jijini Arusha, Mgunda alisema kuwa kwenye mchezo huo wao wanaenda kupambana na Yanga na sio kumuangalia mchezaji mmoja

‘Kwanza. niseme kitu kimoja, hatuchezi na Mayele kesho, tunacheza na Yanga, kama Mayele atakuwa kwenye Yanga tutakutana na Yanga, hautuchezi na mtu,” alisema kocha huyo.

Katika michezo yote miwili ya Ligi Kuu waliokutana kati ya Yanga na Coastal Union, Mayele alifanikiwa kuifunga timu hiyo mabaop 2-0, huku mchezo wa mwisho ukiwa wa kutangazwa ubingwa.

Katika hatua nyingine kocha huyo kuelekea mchezo huo amefunguka kuwa wanawaheshimu Yanga na wamejiandaa na mchezo wa kesho kwa kutambua ubora wa mpinzani wao.

“Tumejiandaa kwa mchezo wa kesho na ndio maana tupo hapa na fainali inajulikana lazima mshindi apatikane na maandalizi ya mchezo huo tayari yameshakamalika,” alisema Mgunda.

error: Content is protected !!