August 12, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mgomo UDSM; Hakijaeleweka

Spread the love

WANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wamegoma kusitisha mgomo wao mpaka pale pesa za kujikimu zitakapoingizwa kwenye akaunti zao, anaandika Faki Sosi.

Mgomo huo umeanzishwa baada ya kucheleweshwa fedha zao za kujikimu zinazotolewa kila baada ya siku 60.

Wanafunzi hao wanadai fedha hizo baada ya kupita siku tano bila kupewa taarifa yoyote ikiwemo kwamba, serikali haina fedha.

Mgomo huo umeanza saa mbili asubuhi ambapo mpaka sasa haujakoma kutokana na msimamo wa wanafunzi hao wa kutoacha kugoma mpaka watakapopatiwa haki yao.

Akizungumza na waandishi wa habari Prof. Rwekaza Mkandara, Makamu Mkuu wa UDSM amesema kuwa, fedha hizo zitatolewa kabla ya kufuka Saa 12 jioni.

Awali msimo wa wasomi hao ni kumtaka Paul Makonda, Mkuu wa Dar es Salaam, Ally Salum Sapi, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni na Boniface Jacob, Meya wa Manispaa ya Kinondoni kuzungumza nao.

Erasmi Leon, Rais wa Serikali ya Wanafunzi  UDSM na Mshangama Shamira, makamu wake wamesema kuwa, mgomo husika utaendelea mpaka pale watakapothibitisha kuwa, fedha zao zimeingia katika akaunti zao.

Wanafunzi wamekusanyika katika eneo la Revolution Square lililopo chuoni hapo kwa amani huku wakiimba nyimbo mbalimbali za uzalendo.

“Kama sio juhudi zako Nyerere…, Sitasimama maovu yakitawala…., Vijana tusilale bado mapambano…. alisema Nyerere vijana wote tumelegea sharti tuanze mchakamchaka….” Wamesikika wakiimba.

Hata hivyo, mpaka muda huu viongozi waliowahitaji kuzungumza nao hawajafika kwenye eneo la tukio.

error: Content is protected !!