Thursday , 28 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Mgomo Kariakoo: Wafanyabiashara wa kigeni waiangukia Serikali
Habari Mchanganyiko

Mgomo Kariakoo: Wafanyabiashara wa kigeni waiangukia Serikali

Baadhi ya maduka ya Kariakoo yakiwa yamefungwa
Spread the love

 

WAKATI mgomo wa kufungua Biashara katika Soko la Kariakoo, jijini Dar es Salaam, ukishika Kasi, baadhi ya wafanyabiashara kutoka nchi jirani wameomba Serikali iumalize ili kuwaepusha na hasara watakazopata kwa kukosa Huduma. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Ombi Hilo limetolewa leo Jumatatu, tarehe 15 Mei 2023, jijini Dar es Salaam, baada ya wafanyabiashara wa Kariakoo kuanzisha mgomo wa kutofungua maduka kwa muda usiojulikana, Hadi malalamiko Yao kuhusu Kodi yatakapofanyiwa kazi.

Akizungumza na MwanaHALISI Online, mfanyabiashara kutoka Zimbabwe, Jeremiah Magwada, amesema mgomo huo endapo utaendelea utawapa hasara ya kifedha kutokana na kukosa Huduma.

“Ninavyokwambia hapa nimeingia Jana usiku kutoka Zimbabwe, nimekuja kufuata mzigo wa nguo na mipango yangu ilikuwa Leo nichukue mzigo kesho niondoke. Lakini hapa nilipo sielewi sababu sijui lini mgomo unaisha ili nipate Huduma niondoke zangu,” amesema Magwada na kuongeza:

“Hasara nitakayopata ni kubwa, itanilizimu kupoteza pesa ya kulipia Huduma za kulala na chakula Hadi pale watakapofungua maduka. Endapo hawatafungua maduka kwa muda wa wiki nzima itanilazimu kuondoka hivyo nitapa hasara ya gharama za usafiri, chakula na malazi.”

Kwa upande wake Alex Chiomba, kutoka Zambia, amesema “kama ningejua Kuna mgomo nisisngekuja, maana kwa Hali hii ni kama nimepoteza fedha zangu. Ninachoomba Serikali ya Tanzania iingilie kati mgomo uishe maduka yafunguliwe.”

Amos Makala, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam

Zephania Obadia, mfanyakazi katika kampuni ya mabasi ya Classic inayofanya safari zake kutoka Tanzania-Zambia Hadi Zimbabwe, amesema mgomo huo unawaathiri.

“Sisi tulipanga kupakiw usiku wa Leo ili kesho afajiri tuanze safari, lakini kwa mgomo huu hatuna uhakika kama basi tutazaja sababu wateja Wetu wengi Hadi sasa tumefanya Mawasiliano Yao hawajapata mzigo,” amesema Obadia.

Miongoni mwa malalamiko ya wafanyabiashara hao ni operesheni zinazofanywa mara kwa mara na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),dhidi ya wateja wanaonunua mizigo sokoni hapo, Kodi mpya ya stoo za kuhifadhia mizigo na Kodi nyinginezo.

MwanaHALISI Online imezungumza na mfanyabiashara ambaye hakutaka kutajwa jina lake, ambaye amedai tangu operesheni za TRA kukamatwa wakamata wateja zianze, zimeathiri biashara zake ambapo wateja wake zaidi ya watano kutoka Zambia, wameacha kuja kununua mzigo kwake.

Wakati hayo yanajiri, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Kariakoo, Martin Mbwana, amesema Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba, atafika sokoni hapo Leo kwa ajili ya kuja kuzungumza na wafanyabiashara ili wasitishe mgomo.

Wafanyabiashara hao wameendelea na mgomo licha ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla, kuwataka waunde Timu itakayokwenda kuzungumza na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, jijini Dodoma Alhamisi ya wiki hii.

Pia, Makalla akiagiza TRA kusitishwa operesheni zake Hadi mgogoro huo utakapopatiwa ufumbuzi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!