August 13, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mgomo Dar, abiria wasota

Spread the love

MAELFU ya abiria leo wamekwama kusafiri baada ya madereva wanaoendesha mabasi yanayofanya safari zake kati ya Buguruni, jijini Dar es Salaam na Kisarawe, Pwani kugoma, anaandika Pendo Omary.

Kugoma kwa mabasi hayo kwa muda usiojulikana kumesababisha usumbufu kutokana na abiria kulazimika kushinda katika Kituo cha Mabasi cha Buguruni na Kile cha Pugu bila kujua hatma ya safari yao kuelekea maeneo ya Vikumboru, Malui, Chole/Kwala na Msanga mkoani Pwani.

Wakizungumza na MwanaHALISI Online baadhi ya madereva hao wamesema, wameamua kuchukua hatua ya kurejesha mabasi hayo kwa wamiliki kwa kile walichokiita ‘maslahi duni’ yanayosababishwa na hujuma inayofanywa na madereva na wamiliki wa magari madogo aina ya Noah zinazofanya safari katika maeneo hayo bila kuruhusiwa na mamlaka za serikali.

“Kituo hichi cha Buguruni kina magari si chini ya 10 na kila gari hubeba abilia 40, hivyo safari ya kwenda pekee tunasafirisha wastani wa abilia 400, bado wanaokuja Dar es Salaam.

“Ni watu wengi leo wamekwama. Tumeamua kurudisha magari kwa matajiri kwa sababu hakuna faida tunayoipata.

“Sababu mkubwa ni kitendo cha vyombo vya serikali kuruhusu magari aina ya Noah kufanya safari katika eneo letu lakazi.

“Tunany’ang’anyana abilia. Wao hawalipi mapato yoyote. Na sisi tunalipa mapato na kwa siku tunatakiwa kuwasilisha hesabu ya Sh. 200,000 kwa tajiri,” amesema Hassan Juma, dereva.

Juma amesema “hawa madereva tukiwauliza kwa nini wanafanya kazi bila kufuata utaratibu, wanajibu kwamba, kila mwezi kuna fungu wanatoa mahali ili waendelee kufanya hiyo kazi.

“Tumepeleka taarifa hizikatika vyombo vya serikali lakini hakuna hatua iliyochukuliwa kila siku tunaambiwa wanashughulikia,” amesema.

Azizi Pazi ambaye ni dereva amesema “hizi taarifa tumepeleka kwa Ofisa Usalama Kibaha, Mkurugenzi wa Kanda ya Ukonga na vyombo vyote vinavyohusika.

“Lakini hakuna majibu yanayoleta suruhu. Askari wa usalama barabarani wanayaona magari hayo yakichukua abiria bila kufuata utaratibu, hawachukui hatua.

“Juzi tu nimefukuzwa kazi. Nadaiwa Sh. 220,000 na tajiri. Watu wanauza hadi aseti za ndani. Yote haya ni kwa sababu tunashidwa kufikisha hesabu inayotakiwa na tajiri, kila siku tunapata hasara. Hivyo tunasisitiza hatujagoma. Ila tumeona ni bora turejeshe magari haya kwa wamiliki,” amesema Pazi.

Grace Mwakangale ambaye ni abilia ameuambia mtandao wa MwanaHALISI Online “Nipo hapa na mizigo yangu tangu saa 12 asubuhi. Nilitaka kuondoka na gari la asubuhi lakini imeshindikana. Hakuna gari linalopakia abilia. Nina shughuli zangu za shamba, mpaka sasa sijui nitafanya nini.”

error: Content is protected !!