TOKYO Sexwale, ambaye ni Mgombea wa urais wa Fifa kutoka Afrika Kusini amejiondoa katika kinyang’anyiro cha uchaguzi wa mrithi wa Sepp Blatter.
Sexwale, akihutubu kabla ya kura kupigwa, amesema hataki kugawanya kura na akawahimiza wajumbe waamue kati ya wagombea wanne waliosalia.
Ameahidi kuunga mkono na kufanya kazi na atakayeshinda. “Nafikisha kampeni yangu kikomo hapa,” amesema.
Wagombea waliosalia ni Sheikh Salman bin Ebrahim al-Khalifa, Gianni Infantino, Mwana mfalme Ali bin al-Hussein, na Jerome Champagne.
More Stories
Injinia Hersi kuanza na uwanja Yanga
Sopu aibuka kinara wa mabao ASFC
Mgunda atoa tahadhari kwa Mayele kesho