May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mgombea uspika ‘awananga’ wenziwe CCM

Spread the love

 

MGOMBEA nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Hamisi Rajabu amewataka wanaCCM wenzake pamoja wabunge kutompitisha mgombea mwenye kashfa ya ufisadi au hulka ya uchu wa madaraka. Anaripoti Danson Kaijage – Dodoma… (endelea)

Rajabu ametoa kauli hiyo leo tarehe 16 Januari wakati akizungumza na MWANAHALISI ONLINE kuhusu tathmini yake katika kinyang’anyiro hicho.

Rajabu ambaye ni miongoni mwa wanachama waliochukuwa fomu ndani ya chama hicho kuomba kuchaguliwa mgombea spika, licha ya kuwa na umri wa miaka 35 ambao ni mdogo kuliko wagombea wote 70 waliorejesha fomu.

Amesema licha ya kwamba ni ukomavu wa kidemokrasia ya watu kuchukua fomu za kuwania nafasi hiyo lakini waliowengi hawawezi kutenda haki kwa wabunge na serikali kutokana na tabia za kuwa na tama za madaraka.

“Unaweza kujiuliza mtu ananafasi ndani ya Bunge lakini anaomba nafasi nyingine sawa siyo tatizo lakini amefanya nini cha kuwavutia watanzania au wanasiasa au ammelinda vipi demokrasia hata ndani ya Bunge? amehoji Rajabu.

Katika hatua nyingine Rajabu amesema kuwa nafasi ya spika haihitaji mtu wa kujipenekeza bali inahitaji mtu ambaye anajiamini kwa kusimamia misingi ya Katiba, sheria na kanuni za Bunge.

“Ukiangalia wote waliochukua fomu za kuomba kuteuliwa kuwania kiti cha spika ni watu ambao hawawezi kusimamia demokrasia ambayo inalalamikiwa kwa sasa kutokana na waliowengi kutanguliza uchama badala ya maslahi mapana ya Watanzania,” amesema.

Aidha, amesema iwapo atapitishwa kuwania nafasi ya uspika hatakuwa tayari kuruhusu michango ya wabunge isiyokuwa na tija kwa wabunge wote bila kujali itikadi za vyama vyao.

Amesema tangu Bunge lilipoanzishwa mwaka 1956 alijawahi kuongozwa na spika kijana na sasa umefika wakati wa kuongozwa na kijana.

Rajabu ambaye ni Mjumbe  wa Halmashauri Kuu CCM Wilaya ya Mkinga na Mjumbe wa kamati ya utekelezaji Baraza la vijana wa chama hicho UVCCM Mkoa wa Tanga, Hamis Rajabu (35) ambaye ni kati ya Makada waliochukua fomu na kurejesha 69 akiwa na umri mdogo kuliko wote.

Rajabu alichukua fomu tarehe 12 Januari 2022, makao makuu ya CCM White House –  jijini Dodoma.

CCM inatafuta mrithi wa Job Ndugai ambaye tarehe 6 Januari 2022, alitangaza kujiuzulu uspika wa Bunge.

Mchakato wa uchukuaji fomu ulianza tarehe 10 hadi 15 Januari 2022, kisha taratibu zingine ndani ya chama hicho zitaendelea kumpata mgombea mmoja.

Zaidi ya wanachama 20 wamekwisha kujitokeza kuchukua fomu wakiwemo vigogo wa Bunge.

error: Content is protected !!