
MGOMBEA Urais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Flaviana Charles amemwomba Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kuhakikisha uhuru wa wanahabari, kujieleza na kukusanyika unalindwa na kupewa kipaumbele. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Flaviana amesema hayo katika mahojiano maalum na MwanaHALISI TV, kuhusu dhamira yake ya kuwania urais wa TLS, katika uchaguzi mkuu, utakaofanyika tarehe 15 Aprili 2021, jijini Arusha.
Flaviana ni miongoni mwa wagombea watano wa nafasi hiyo ya juu, akiwa mwanamke pekee ambaye amezungumzia mikakati mbalimbali ikiwemo, alivyojipanga kulinda maslahi ya wanachama wa TLS, ujumbe atakaompa Rais Samia iwapo atakutana naye na jinsi wanawake wanavyoweza kuongoza na heshima kwa wanaume.

Je, unatambua, Flaviana ambaye ni Katibu wa Chama cha Wanasheria Afrika aliwahi kugombea ubunge wa viti maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)? Unajua kasema nini kutenganisha maslahi ya TLS?
Mengi zaidi kuhusu alichokizungumza, fuatilia mahojiano hayo
More Stories
Rais Samia apokea tuzo ya Babacar Ndiaye, amtaja Magufuli
Mbunge Ditopile awapigania wavuvi
Msajili wa vyama ampiga ‘Stop’ Mbatia NCCR-Mageuzi