August 13, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mgombea urais alia kunyanyaswa kingono, abwatuka

Spread the love

 

UNYANYASAJI wa kingono sasa unaonekana kumuathiri mtu yeyote bila ubaguzi wakiwemo wagombea urais. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa… (endelea)

Tukio hilo la aina yake limetokea juzi tarehe 29 Julai, 2022 baada ya mgombea urais katika Uchaguzi Mkuu nchini Kenya kupitia chama cha Roots Party, Profesa George Wajackoyah kulazimika kusimamisha hotuba yake kwa muda baada ya mfuasi wake mmoja kumgusa sehemu zake za siri.

Wajackoyah ambaye alikuwa amevaa suruali ya michezo, T-shati ya kijani na durag kichwani kama ilivyo kawaida yake alikuwa amesimama juu ya lori huku akiwahutubia wafuasi wake wakati tukio hilo lilitokea.

“… na mimi nimekuja nikasema..” Wajackoyah alisikika akisema katika klipu ya video inayosambaa mitandao ya kijamii kabla ya mguso wa ghafla kwenye sehemu zake za siri kumkatiza kuendelea kuhutubia.

“Usinishike hivyo!”… sasa huyu ananishika sehemu yangu ya nyeti!” mgombea urais huyo ambaye alionekana kukerwa na kitendo hicho alisikika akilalamika.

Video ya tukio hilo ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii huku wanamitandao wakitoa maoni mbalimbali.

Baadhi ya wanamitandao walifanya mzaha na tukio hilo wakidai kuwa huenda shabiki huyo aliamua kufuata kauli mbiu ya Root Party ya ‘Tikisa mti’.

error: Content is protected !!