Monday , 11 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mgombea ubunge CCM kuwarejesha nyumbani wana Mufundi
Habari za Siasa

Mgombea ubunge CCM kuwarejesha nyumbani wana Mufundi

Spread the love

MGOMBEA Ubunge wa Mufindi Kusini Mkoa wa Iringa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), David Kihenzile amesema, vijana na wasomi wote wanaoishi nje ya Mufindi wanapaswa kurudi nyumbani na kuijenga Mufindi kimaendeleo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mufindi … (endelea).

Kihenzile amesema hayo jana Jumapili tarehe 6 Septemba 2020 wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi katika jimbo hilo uliofanyika uwanja wa shule ya msingi Igowole kata ya Igowole wilayani Mufindi.

Alisema atajitahidi vijana wenye uwezo wanaotokana na jimbo la hilo kukumbuka na kurudi nyumbani kuijenga Mufindi yao.

“Wapo wenzetu wa Mufindi wapo katika nafasi kubwa na wengine wameaminiwa serikalini hivyo tuwatumie na wao wakumbuke kurudi kuijenga Mufindi yao ili kuwasaidia wananchi wanaoishi jimboni kuona manufaa ya watoto wao waliowasomesha na kupata ajira nje na ndani ya Iringa,” alisema Kihenzile.

Alisema wapo vijana wengi katika jimbo hilo wana ajira wanauwezo na wanauzoefu na wengine hawana uzoefu tutajitahidi kuwatambua wako wapi hata kama wapo nje ya Mufindi tutahakikisha tunahangaika kutafuta fulsa za kuwasaidia ndani ya jimbo hilo.

Kihenzile alivitaja vipaumbele vyake ni pamoja na barabara, elimu, maji, afya, kilimo, ufugaji, umeme na michezo ikiwemo kurudisha mashindano ya Muungano Cup pamoja na kuanzisha ‘Mufindi day’ ili kuwakutanisha vijana wazee na watoto katika jimbo hilo.

“Nitakuwa mtiifu na mnyenyekevu kwa wazee, nitakuwa kimbilio la kinamama na makundi maalum na zaidi nitakuwa rafiki wa vijana ili jimbo letu liwe kitu kimoja,” alisema Kihenzile.

Akizindua kampeni hizo mjumbe wa halmashauri kuu taifa, Salmu Abri Asas alisema, Rais John Magufuli amefanya maendeleo makubwa kwa muda mfupi jambo ambalo wananchi wanapaswa kumchagua tena ili amalizie mambo mengine mazuri zaidi.

 

“Nchi yetu imetambulika kimataifa zaidi kupitia Rais wetu na tunaomba Watanzania wote wampigie kura ili aendelee kutufanyia mengi mazuri ambayo watanzania wanayahitaji katika nchi hii,” alisema.

Kwa upande wake, aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Mendrad Kigola alisema anamkabidhi kijiti David Kihenzile ahakikishe analeta maendeleo katika jimbo hilo na kumalizia yale aliyoyaacha bila kumalizika.

“Naomba ukawaunganishe wana Mufindi Kusini na kitu kimoja kwa maendeleo ukamalizie mipango ya kimaendeleo ambayo mimi nimeiacha haijamalizika ili wananchi wawe katika hali nzuri,” alisema Kigola.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Jaji Kiongozi akerwa wananchi kukosa imani na mahakama

Spread the loveWATENDAJI wa Mahakama ya Tanzania, wametakiwa kuweka mikakati itakayosaidia kurejesha...

BurudikaHabari za Siasa

Samia amchangia Professa Jay mil. 50, Chadema, wasanii wamwaga manoti

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amechangia kiasi cha Sh 50 milioni...

Habari za Siasa

Biteko: Samia ni muumini wa maridhiano sio kwa kuigiza

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Mpango: Sitakufa bali nitaishi

Spread the loveMAKAMU  wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk....

error: Content is protected !!