June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mgombea Mbagala alia na udini wa CCM

Spread the love

MGOMBEA ubunge Jimbo la Mbagala, Kondo Bungo amefunga kampeni zake za kwa kuwata wananchi wamchague yeye na madiwani wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), pamoja na mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA, Edward Lowassa. Anaandika Faki Sosi … (endelea).

Akizungumza katika viwanja wa Zakhiem Mbagala Jijini Dar es Salaam, amesema kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kimewabagua wananchi kwa muda mrefu sasa kutokana propaganda wanazoeneza.

Propaganda hizo ni pamoja na kuwaaminisha wananchi kuwa chama cha Demokrasia na Maendeleo ni chama cha wakristo huku chama cha wananchi CUF kikitajwa kuwa ni cha Waislam .

Amesema kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wa Taifa (NEC) ikiharibu utaratibu watu wa Mbagala hawataweza kuvumilia endapo kutakuwa na wizi wa wazi.

Amesema kuwa anawashukuru viongozi wa dini zote kwa ushirikiano wao katia kuhakisha anatwaa jimbo hilo la Mbagala na ndio waliowaombea dua makada wake katika kuhakisha kuwa hawaibiwi kura zake.

error: Content is protected !!