July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mgombea Chadema kujenga sekondari ya mfano

Spread the love

MGOMBEA ubunge wa jimbo la Arumeru Magharibi kupitia Chadema, Gibson Meiseyeki amesema kuwa endapo atachaguliwa kuongoza jimbo hilo atahakikisha anajenga shule ya sekondari ya mfano katika kata ya Kiutu, Arumeru. Anaandika Ferdinand Shayo, Arumeru … (endelea).

Aliyasema hayo jana wakati akizungumza na wananchi wa kata hiyo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata hiyo.

Meiseyeki amesema kuwa, jimbo hilo limekuwa likikumbana na changamoto mbalimbali ya ubovu wa madarasa pamoja na kutokuwa na madawati ya kutosha mashuleni, hali inayochagia kuendelea kuwepo kwa utoro kwa wanafunzi kutokana na mazingira magumu wanayosomea.

Amesema atahakikisha anaboresha elimu katika kata hiyo na jimbo kwa ujumla kwa kuwa na shule za mfano wa kuigwa na kuwawezesha wanafunzi kuwa na moyo wa kusoma kutokana na kujengewa mazingira mazuri yanayoridhisha.

“Inashangaza katika jimbo hili, hatuna hata barabara ya futi mbili ya lami na hela zipo za kutosha halmashauri, tatizo ni kuongozwa na viongozi wasiojali maslahi ya wananchi. Nipeni kura niwaletee mabadiliko makubwa, kamwe hamtajutia kunichagua,” amesema Meiseyeki.

Alifafanua atahakikisha kuwa ananunua makatapila kwa ajili ya kutengeneza barabara za jimbo hilo ili ziwe zinazopitika wakati wote.

Amesema anaweka lami katika barabara ya Mount Meru kwenda Olgilai, kufanikiwa hilo amewataka wananchi wanamchagua Rais, mbunge na diwani wa Chadema ili wanufaike na fursa mbalimbali ikiwemo elimu bure.

Meseiyeki amesema atatoa elimu ya ujasiriamali kwa wanawake na vijana ili kuwawezesha kutumia fedha za mkopo watakazopata wazitumie kwa malengo yaliyokusudiwa ili kujikwamua kiuchumi.

Naye Mgombea udiwani wa kata ya Kiutu, Zephania Sirikwa amewataka wananchi wa kata hiyo kumchagua ili awaletee mabadiliko ya kweli katika kata hiyo.

error: Content is protected !!