Wednesday , 27 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mgombea Chadema amwangushia jumba bovu mgombea CCM
Habari za Siasa

Mgombea Chadema amwangushia jumba bovu mgombea CCM

Spread the love

CONCHESTA Rwamlaza, mgombea ubunge katika Jimbo la Bukoba vijinini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), amemtuhumu Jason Rweikiza, mgombea mwenzake kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwamba ‘hafai’ kwani amewapuuza wananchi wake. Anaripoti Danson Kaijage, Bukoba … (endelea).  

Akizungumza kwenye kampeni zake katika Kata ya Kanyangereko, amesema wananchi wa kata hiyo hawana sababu ya kumchagua kwa kuwa, walimpa nafasi kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, lakini ameshindwa kuwapelekea maendeleo ikiwemo kuwawashia umeme.

Amesema, wananchi hao hususani Kijiji cha Kigusha, hawapaswi kumrejesha mtu ambaye tayari walimpa nafasi na akawaangusha.

Pia Conchesta amesema, Jimbo la Bukoba Vijijiji limekuwa nyuma kimaendeleo kutokana na kutopata kiongozi sahihi kwa ajili ya maendeleo.

Amesema, viongozi na wabunge wanaopatikana kwenye jimbo hilo, wameshindwa kuwatetea wananchi badala yake wamekuwa wakijinufaisha wenyewe.

“Badala ya kuwatumikia wananchi, wanajikusanyia wenyewe na wanatumikia chama chao, ndio maana jimbo hili limebaki kama lilivyo miaka yote,” amesema.

Katika kampeini zake Conchesta amesema, iwapo atapata ridhaa ya kuwa mbunge wa jimbo hilo, atahakikisha anaibana serikali ili iweze kuboresha bei ya mazao hususani Kahawa,Ndizi pamoja na majani ya chai ili kuweza kuboresha maisha ya wakulima.

Amesema, Kata ya Ruhunga wanatumia maji machafu ambayo yamejaa tope hivyo, miongoni mwa majukumu yake ni kuhakikisha anabadili maisha hayo.

Amewataka wananchi wa jimbo hilo kumpa kura, ili akasimamia matamanio ya maendelea ambayo wameshindwa kuyapata kutokana na kukosa mwakilishi sahihi.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

Habari za Siasa

Mgongano wa kimasilahi wamhamisha Chande TTTCL

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),...

Habari za SiasaTangulizi

Mgawo wa umeme: Rais Samia ampa miezi sita bosi mpya TANESCO

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amempa miezi sita Mkurugenzi...

Habari za Siasa

Rais Samia avunja bodi ya REA

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Balozi Jacob Kingu, kuwa...

error: Content is protected !!