July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mgombea Chadema alia na ‘bao la mkono’

Spread the love

MGOMBEA ubunge wa jimbo la Bukombe kupitia Chadema, Prof. Kulikoyela Kahigi amelalamikia rafu zinazofanywa na wagombea wa CCM kuwahonga wananchi. Anaandika Dany Tibason, Bukombe … (endelea).

Prof. Kahigi ameliambia Mwanahalisi Online kuwa kwa sasa hali ni mbaya kutokana na wagombea wa chama tawala kumwaga fedha kwa wananchi ili wakichagua chama hicho.

Amesema vitendo vya utoaji hongo kwa wananchi vinafanywa waziwazi kutokana na upinzani kuonekana kuwa unanguvu katika jimbo hilo.

Akizungumzia jambo hilo amesema kwa sasa viongozi wa CCM wameona kuwa hawakubaliwi kwa wananchi sasa wameamua kuibuka na mtindo mpya ya kumwaga hela kwa wananchi.

Mbali na hilo Prof. Kahigi amesema wilaya ya Bukombe ni miongoni mwa wilaya zilizoweza kupata maendeleo kwa kipindi cha miaka mitano baada ya kuiongoza.

Prof. Kahigi alibainisha baadhi ya maendeleo kuwa ni pamoja na ujenzi wa nyumba za walimu, uchimbaji wa visima vya maji, upatikanaji wa Umeme, ukarabati wa vyumba vya madarasa pamoja na kupanda kwa elimu shule ya msingi na sekondari.

Amesema kwa miaka zaidi ya 50 wilaya ya Bukombe na mkoa wa Geita kwa ujumla elimu ilishuka sana tofauti na ilivyo sasa kwani katika wilaya ya Bukombe imeweza kushika nafasi ya 11 kati ya Halmashauri 152 huku shule za sekondari zikishika nafasi ya pili kitaifa.

Mbali na hilo amesema wilaya ya Bukombe imeweza kuanzisha Ujenzi wa soko la kimataifa.

Kwa hatua nyingine viongozi wa CCM pamoja na wagombea wa ngazi mbalimbali walipotafutwa kwa nyakati tofauti wamesema wao wanaendelea na kampeni wala hawana haja ya malumbano.

error: Content is protected !!