Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mgombea Chadema adundwa, anyang’anwa fomu
Habari za Siasa

Mgombea Chadema adundwa, anyang’anwa fomu

Spread the love

LUCAS Nyangindu, mgombea uenyekiti wa kijiji cha Mwatanga, Kishapu mkoani Shinyanga kupitia Chadema, amepigwa na kunyang’anywa fomu baada ya kuwekwa chini ya ulinzi na mgambo wa kijiji hicho. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Taarifa zaidi kutoka kwenye kijiji hicho zimeeleza, Nyangindu baada ya kupokea kipigo hicho, alikabidhiwa kwa polisi bila kuelezwa tuhuma zake.

Even Noah, Ofisa wa Tarafa ya Kishapu ndiye aliyotoa amri ya Nyangindu kukamatwa. Hata hivyo, hakueleza sababu za kutoa amri hiyo ingawa alikiri kutoa amri hiyo.

Alipobanwa zaidi kueleza sababu za kutoa amri hiyo, alisema “siwezi kuongelea hizo zaidi kwa sasa.”

Zacharia Obadi, Katibu wa Chadema Mkoa wa Shinyanga, ameuambia mtandao huu, kwamba mgombea wake alivamiwa na kuanza kushushiwa kipondo muda mfupi baada ya kukabidhiwa fomu.

“Wakati anapigwa alikuwa na fomu alizochukua kwa ajili ya kugombea, hizo fomu nazo walimnyang’anya. Hawakutaka kueleza sababu za kipigo kile,” amesema na kuongeza “baada ya kipigo hicho, alichukuliwa na polisi na kupelekwa kituoni.”

Martine Ndamo, msimamizi wa uchaguzi wa serikali za mitaa Kishapu amesema, taarifa za kipigo cha mgombea huyo amezipata na kwamba anaendelea kufuatilia.

Hata hivyo, ameelezwa kuchukizwa na hatua ya Ofisa Tarafa kuingilia masuala ya uchaguzi na kuagiza vitendo vya kihuni kufanywa dhidi ya mgombea.

“Ofisa Tarafa kikanuni hana mamlaka katika masuala ya uchaguzi, nimeshtushwa sana na taarifa hizo hasa kusikia yeye anahusika,” amesema.

Fomu kuelekea uchaguzi huo zimeanza kutoewa jana tarehe 29 Oktoba 2019, ambapo umepangwa kufanyika tarehe 24 Novemba mwaka huu, huku kampeni zikitarajiwa kuanza tarehe kuanzia 17 hadi 23 Novemba.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!