Monday , 11 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mgombea CCK akwama kugombea urais Tanzania
Habari za Siasa

Mgombea CCK akwama kugombea urais Tanzania

Spread the love

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), haijamteua David Mwaijojele wa Chama Cha Kijamii (CCK) kuwa mgombea urais wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano 28 Oktoba 2020 baada ya kushindwa kukidhi masharti yaliyowekwa kwa mujibu wa Katiba na sharea. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea)

Mwaijojele ambaye ni Mwenyekiti wa chama hicho, ameshindwa kuteuliwa leo Jumanne tarehe 25 Agosti 2020 na Mwenyekiti wa NEC, Jaji Semistocles Kaijage baada ya kuwasili ofisi za tume hiyo jijini Dodoma akiwa peke yake.

Katibu wa NEC, Dk. Willson Mahera amesema, baadhi ya masharti aliyoshindwa kukidhi ni kutokujazwa fomu namba 10 ya mgombea mwenza na picha za mgombea mwenza.

Kwa upande wake, Mweneykiti wa NEC, Jaji Semistocles Kaijage amesema tume hiyo imeshindwa kumteua David Mwaijojele kuwa mgombea wa urais baada ya kutokukidhi masharti ya Katiba na sheria za uchaguzi.

Mwaijojele amekuwa mgombea wa kwanza kati ya 17 kutokuteuliwa kugombea nafasi ya juu ya uongoza wa Tanzania kati ya wagombea 12 waliorejesha na kuteuliwa.

Tofauti na vyama vingine 12, Mwaijojele amewasili ukumbini akiwa peke yake tofauti na wagombea wengine waliowasili akiwa na viongozi na wanachama wa vyama hivyo.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online, MwanaHALISI TV na mitandao yetu ya kijamii kwa taarifa na habari mbalimbali

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Jaji Kiongozi akerwa wananchi kukosa imani na mahakama

Spread the loveWATENDAJI wa Mahakama ya Tanzania, wametakiwa kuweka mikakati itakayosaidia kurejesha...

BurudikaHabari za Siasa

Samia amchangia Professa Jay mil. 50, Chadema, wasanii wamwaga manoti

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amechangia kiasi cha Sh 50 milioni...

Habari za Siasa

Biteko: Samia ni muumini wa maridhiano sio kwa kuigiza

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Mpango: Sitakufa bali nitaishi

Spread the loveMAKAMU  wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk....

error: Content is protected !!