May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mgogoro wakulima, wafugani Ruaha kufika tamati

Dk. Damas Ndumbalo

Spread the love

 

UTATUZI wa mgogoro wa muda mrefu kati ya wakulima na wafugaji wanaozunguka Hifadhi ya Taifa Ruaha, upo mbioni kuanza. Anaripoti Mwandiahi Wetu, Dodoma … (endelea).

Waziri wa Maliasil na Utalii Dk. Damas Ndumbaro ametoa kauli hiyo leo tarehe 16 Aprili 2021, bungeni jijini Dodoma akijibu swali la Francis Leonard Mtega, Mbunge wa Mbarali.

Mtega alitaka kujua mkakati wa serikali kumaliza migogoro kati ya wakulima na wafugaji wanaozunguka hifadhi hiyo.

“Serikali iliunda kamati iliyojumuisha mawaziri kutoka wizara nane kwa ajili ya kufuatilia na kutatua migogoro ya ardhi nchini. Migogoro iliyofanyiwa kazi na kamati husika ni pamoja na migogoro kati ya wakulima na wafugaji wanaozunguka Hifadhi ya Taifa Ruaha.

“Kamati hiyo imeshafanya tathmini ya migogoro hiyo na kutoa mapendekezo ambayo yameshatolewa maamuzi na Baraza la Mawaziri kwa ajili ya utekelezaji utakaoanza hivi karibuni,” amesema.

Waziri Ndumbaro ameomna wabunge ambao maeneo yao yana changamoto ya migogoro, kutoa ushirikiano wakati wa utekelezaji wa maamuzi ya Baraza la Mawaziri.

error: Content is protected !!