Saturday , 20 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Mgogoro wa Kenya, Somalia kuhusu mpaka wa baharini wazidi kutokota
Kimataifa

Mgogoro wa Kenya, Somalia kuhusu mpaka wa baharini wazidi kutokota

Spread the love

 

MGOGORO wa kuwania eneo la pembe tatu lililopo katika bahari ya Hindi kati ya mataifa ya Kenya na Somalia umezidi kutokota baada ya Serikali ya Kenya kulaani na kukataa uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa kuhusu haki (ICJ), ambayo ilitoa uamuzi wa sakata hilo na kuipendelea zaidi Somalia. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Katika taarifa iliyotolewa kwa umma na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amelaani uamuzi wa Mahakama hiyo yenye makao yake mjini Hague nchini Uholanzi na kusema serikali yake inakataa kwa nguvu zote uamuzi huo na kusisitiza kuwa kama kiongozi wa Kenya, atahakikisha kuwa mipaka ya eneo hilo la Bahari inalindwa kama ambavyo imekuwa tangu mwaka 1979.

Aidha, Kenyatta amesema, uamuzi wa Mahakama hiyo utaharibu uhusiano kati ya nchi yake na Somalia na kurudisha nyuma mafanikio yaliyopatikana kijamii, kiuchumi na kisiasa na anataka sintofahamu hiyo kutatuliwa kidiplomasia.

 

Uhuru Kenyatta

“Kenya inaendelea kushinikiza suluhu ya kidiplomasia kutatua sintofahamu hii, kwa hivyo Wakenya wenzangu, niwahakikishie kuwa kama rais wenu, kuwa tuna nia ya kutatua suala hili kwa maelewano, nawaomba muwe watulivu, wakati huu tunapoendelea kutathmini kwa kina suala hili.” amesema rais Kenyatta.

Aidha, akilihutubia taifa kupitia Televisheni, Rais wa Somalia, Mohamed Abdullahi Mohamed maarufu kama Farmoja, amesema nchi yake imekubali uamuzi wa mahakama hiyo na kuitaka Kenya, kuheshimu uamuzi wa mahakama ili kuimarisha tena uhusiano kati ya nchi hizo jirani.

“Kenya inastahili kuona uamuzi wa mahakama kama fursa ya kuimarisha uhusiano wa nchi hizi mbili. Somalia haikuchagua kuwa jirani na Kenya, lakini yalikuwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu ili tuishi kwa amani na jirani zetu. Somalia ilidhamiria hilo siku zote na inalikaribisha hilo,” amesema rais Farmajo.

Kesi hiyo ilihusu pembetatu ya kilomita za mraba 38,000 katika Bahari ya Hindi ambayo inaaminiwa kuwa na utajiri wa mafuta na gesi.

Tayari Kenya ilikuwa imekata kibali kwa kampuni ya nishati ya ENI kutoka Italia kuanza shughuli za upatikanaji wa rasilimali hiyo, hatua ambayo iliikera Somalia.

Rais Somalia, Mohamed Abdullahi Mohamed

Uamuzi wa Mahakama hiyo ya ICJ hauwezi kukatiwa rufaa, lakini chombo hicho cha sheria hakina namna ya kutekeleza maamuzi yake.

Haifahamiki mpaka sasa kitakachotokea baada ya Kenya kusema haitambui Mahakama hiyo na uamuzi wake.

Mwaka 2009, nchi hizo mbili zilikubaliana katika hati ya makubaliano, ikiungwa mkono na UN, kumaliza mzozo wa mipaka kupitia mazungumzo.

Lakini miaka mitano baadaye, Somalia ilisema mazungumzo yalishindwa na badala yake ikaenda kwa ICJ.

Mwaka 2014, Somalia iliamua kutafuta ufumbuzi wa mzozo huo katika mahakama ya kimataifa ya (International Court of Justice).

Katika ombi lake, Somalia ilisema mazungumzo ya kidiplomasia yameshindikana na sasa mahakama iamue uratibu sahihi wa kijiografia wa mpaka mmoja wa baharini katika Bahari ya Hindi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!