March 8, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mgogoro wa ardhi waibuka upya Karagwe

William Lukuvi, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi

Spread the love

MAMIA ya wananchi wa kijiji cha Chabuhora, wilayani Karagwe, mkoani Kagera, wanahitaji msaada wa haraka wa chakula, baada ya mashamba na nyumba zao kuchomwa moto katika kinachoitwa, “operesheni maalum ya mkuu wa wilaya hiyo, anaandika Joseph Sekiku.

Taarifa kutoka Karagwe zinasema, mkuu huyo wa wilaya aliamua kuchomwa moto nyumba na  mashamba hayo ya wananchi, kwa madai ya kutaka kuwabeba wafugaji.

Taarifa zinasema, wananchi wanaoishi katika maeneo hayo, wamekuwapo kwa miaka kadhaa sasa; wanamiliki maeneo hayo kwa kibari cha serikali ya kijiji.

“Lakini mkuu wa wilaya amefika hapa. Ameanza kuchoma moto nyumba za wananchi na kuwahamisha kwa nguvu.

Anadai sisi ni wavamizi, wakati tumemilikishwa maeneo hayo na serikali za kijiji na tumekuwapo hapa tangu enzi na enzi,” ameeleza mzee mmoja wa makamo kwa sharti la kutotajwa jina.

Anasema, serikali  wilayani humo imekuwa ikidai kuwa wananchi hao wameondolewa katika maeneo hayo kutokana na kuvamia vyanzo vya maji.
Anasema, “serikali ya kijiji imetoa ardhi kwa kaya zile ili waishi na walime.

Hata stakabadhi wanazo. Lakini sasa wameondolewa katika eneo hilo na kuwacha wapweke. Mvua za masika zimeanza na wananchi hawa hawana pa kulala na hawana chakula.”

error: Content is protected !!