Friday , 1 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mgogoro Poli Tengefu la Loliondo wadumu miaka 25
Habari za Siasa

Mgogoro Poli Tengefu la Loliondo wadumu miaka 25

Makundi ya Ng'ombe yaliyokutwa katika Poro Tengefu la Loliondo
Spread the love

MBUNGE wa Viti Maalum, Catherine Magige (CCM) amehoji kuhusina na ni lini serikali itatatua mgogoro wa Pori Tengefu la Loliondo uliodumu zaidi ya miaka 25, anaandika Dany Tibason.

Akiuliza swali leo bungeni, Catherine alidai kuwa katika Pori Tengefu wa Loliondo kumekuwa na mgogoro mkubwa hivyo ni lini serikali itatatua mgogoro huo.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Ramo Makani amesema Desemba 2016, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alifanya ziara katika Wilaya ya Ngorongoro ambapo pamoja na mambo mengine alitoa maelekezo ya jinsi ya kupata ufumbuzi wa mgogoro huo.

Amesema katika utelekezaji wa agizo hilo kamati maalum shirikishi inayoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha ambapo iliundwa ili kupata mapendekezo ya namna ya kutatua migogoro hiyo.

‘’Kamati maalum ilifanya kazi yake kwa njia mbalimbali zikiwemo kufanya vikao na wadau mbalimbali kutembelea eneo lenyewe ili kujua hali halisi na kuandaa taarifa yenye mapendekezo ya namna kutatua mgogoro huo,’’ amesema

Naibu Waziri huyo amesema mapendekezo ya kamati hiyo yamewasilishwa kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Rais Mwinyi kuzikwa Machi 2 visiwani Unguja

Spread the loveMWILI wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Pili wa Tanzania,...

Habari za SiasaTangulizi

Rais mstaafu Mwinyi afariki dunia

Spread the loveRais Mstaafu wa awamu ya pili wa Tanzania, Ally Hassan...

Habari za Siasa

Waziri mkuu Ethiopia atua Tanzania

Spread the loveWaziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la Ethiopia,...

Habari za Siasa

Babu Owino: Vijana msibaki nyuma

Spread the loveMbunge wa Embakasi Mashariki nchini Kenya, Paul Ongili Owino maarafu...

error: Content is protected !!