MGOGORO mwingine umelikumba Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), baada ya wachungaji watatu wa Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, kumtuhumu Askofu wao, Dk Msafiri Mbilu. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).
Taarifa kutoka ndani ya Dayosisi hiyo yenye makao yake makuu, Handeni, Tanga zinasema mgogoro wa sasa, unatokana na makovu ya uchaguzi wa Askofu, ambapo upande mmoja unataka kulipiza kisasi dhidi ya mwingine.
Kwa mujibu wa barua ya wachungaji hao – Dk Eberhardt Ngugi, Dk Anneth Munga na James Mwinuka – Tume iliyoundwa na Askofu Mbilu, kuwahoji kwa tuhuma mbalimbali, tayari imepewa maelekezo ya kuwashughulikia, jambo ambalo hawako tayari kuliona likitendeka.
“Baba Askofu, kwa njia ya barua hii, tunapenda ifahamike kwamba hatuko kinyume na mwito wa kuhojiwa na Kamati, lakini hatuna imani na Tume Maalumu ya Halmashauri Kuu iliyoundwa,”
Soma kwa kina, habari hii katika Gazeti la Raia Mwema, toleo la leo Jumatatu, tarehe 6 Desemba 2021.
Leave a comment