July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mgogoro huu ni hatari kwa usalama

Spread the love

WANAKIJIJI wa Kisana Kata ya Kyebetembo Wilaya ya Muleba Mkoa wa Kagera wameiomba Serikali kuyakomesha mapigano yanayoendelea kati yao na Wanyarwanda wanao saidiwa na serikali wilayani mkoani humo. Anandika Faki Sosi … (endelea).

Akizungumza na wanahabari mmoja wa wahanga wa mapigano hayo Martin Ruzaria amesema mapigano hayo yalianza Januari 12 mwaka huu ambapo Wanyarwanda walivamia kwenye kijiji hicho na kuanza kupiga watoto na wanawake pamoja na kuchoma moto nyumba na ghara za vyakula kijijini hapo.

Amesema mara baad ya uvamizi huo ndipo wakazi wa kijiji hicho na wavamizi hao walipoanza kushambuliana na kusababisha hasara kubwa katika jamii husika.

Amesema mapigano hayo yamesababisha upotevu Ng’ombe 100 na mtu mmoja kupoteza maisha baada ya hali hiyo polisi waliwakamata jamii ya kisukuma na kuwaacha Wanyarwanda.

Amesema ofisi ya mwenyekiti wa kijiji hicho ipo umbali wa kilometa 27 toka eneo la tukio lakini habari zilipomfikia mwenyekiti wa kijiji hicho alituma watu ili kujua kinachoendelea ambapo watu waliotumwa na mwenyekiti huyo walikamatwa na jeshi la polisi.

Amesema kuwa Diwani wa kata Kyebetembo anayefahamika kwa jina la Vedasko Lukunwa amekataa kuwasaidia wananchi kwa madai ya kuwa hawana fedha na kutoa kauli ambazo sio za kizalendo ya kwamba “kheri ukae na wanyarwanda 20 kiliko msukuma mmoja kwani hawana fedha” amesema.

Deus Kajuna pia ni miongoni mwa wahanga wa mapigano hayo aliyeambatana na wenzake hadi Jijini Dar es Salaam amesema kuwa viongozi wa wilaya wameshindwa kusaidia kuumaliza mgogoro huo badala yake namekuwa na dharau kwa jamii hiyo.

Amesema hana imani na Diwani,Ofisa mtendaji wa kata mkuu polisi kata na wilaya pamoja na mkuu wa wilaya ya Mureba.

Amesema wamekuja hapa jijini kama wawakilishi wa wanakijiji hao ambo wamepuuzwa na viongozi hao wa Wilaya na Mkoa.

error: Content is protected !!