Tuesday , 23 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Mgodi wa Barrick wapigwa faini bilioni moja uchafuzi wa mazingira Mara
Habari Mchanganyiko

Mgodi wa Barrick wapigwa faini bilioni moja uchafuzi wa mazingira Mara

Spread the love

KAMPUNI ya Uchimbaji Mkubwa wa Madini ya Dhahabu wa Barrick kupitia mgodi wake wa Barrick North Mara umepigwa faini ya shilingi bilioni moja baada ya kutokea uzembe uliosababisha bomba la maji taka kupasuka na kutiririkia kwenye vyanzo vya maji na makazi ya watu. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akizungumza katika tukio hilo jana tarehe 24 Aprili, 2022 mkoani MaraWaziri wa Madini Dk. Doto Biteko amesema Mgodi wa North Mara unaomilikiwa na Kampuni ya Barrick kwa asilimia 84 na Serikali kwa asilimia 16 unapaswa kuwa mfano bora kwa kufuata na kusimamia sheria, taratibu na kanuni zilizowekwa na serikali.

“Haiwezekani Bomba la maji taka lipasuke saa tatu asubuhi halafu uongozi upate taarifa saa sita mchana na isitoshe kuna walinzi wanaozunguka maeneo hayo, huu ni uzembe wa hali ya juu, sisi tunataka usalama wa watu wetu,” amesema Dk. Biteko.

Aidha, Dk. Biteko amembadilishia majukumu Afisa Migodi Mkazi wa Mgodi wa North Mara baada ya kushindwa kusimamia majukumu yake ipasavyo katika eneo alilopangiwa.

“Kutokana na uzembe huu uliofanyika hapa mgodini naanza na Afisa wangu namuondoa hapa ataenda kupewa majukumu mengine, siwezi kukubali uzembe huu uendelee,” amesema Dk. Biteko.

Sambamba na hayo, Waziri Biteko ameitaka Kampuni ya Barrick kuhakikisha inachangia katika kuleta maendeleo kwa jamii (CSR) ili wananchi wanaoishi katika maeneo yanayozunguka Migodi yaweze kunufaika na uwepo wa mgodi huo katika maeneo yao.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dk. Samuel Gwamaka amesema, Kifungu cha 187 cha Sheria ya Mazingira kinampa mamlaka ya kuipiga faini yenye makosa ya kuvujisha maji taka kuanzia milioni 50 mpaka bilioni 10.

“Kampuni hii ya Barrick tumeipiga faini ya bilioni moja ili iwe mfano kwa wengine, hivyo itambuliwe hilo ni kosa na sisi kama NEMC tutaendelea kufanya ukaguzi wa mara kwa mara ili kuhakikisha makosa kama haya hayajitokezi,” amesema Dk. Gwamaka.

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Ally Happy amesema, Rais Samia Suluhu Hassan anataka kuona fedha zinatolewa kwa ajili ya miradi inawanufaisha wananchi ambapo ameitaka kampuni ya Barrick kutoa michango yake kwa jamii (CSR) ili kusogeza maendeleo kwa jamii.

Pia, Mbunge wa Musoma Vijijini, Mwita Waitara (CCM) amempongeza Dk. Biteko na kusema tatizo la kupasuka kwa bomba la maji taka limetokea jana lakini leo Waziri mwenye dhamana amefika eneo la tukio, hiyo inaonyesha ni kiasi gani anajali na anathamini utu wa watu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NMB yadhamini Mkutano Mkuu ALAT, kufunguliwa na Samia

Spread the loveBENKI ya NMB, imekabidhi hundi yenye thamani ya Sh. 120...

Habari Mchanganyiko

DC ampongeza Dk. Rose Rwakatare kwa kusaidia waathirika wa mafuriko Mlimba

Spread the loveMWENYEKITI wa Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk.  Rose Rwakatare...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mipango na uwekezaji kutumia bilioni 121.3, mradi wa Bagamoyo wapewa kipaumbele

Spread the loveWIZARA ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, imeliomba Bunge...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mbunge ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the loveMBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze kasi...

error: Content is protected !!