July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mgimwa: Tutalipa kifuta jasho

mazao la Alizeti

Spread the love

WANANCHI walioharibiwa mazao yao na wanyamapori hawatalipwa fidia bali watapewa kifuta jasho, Serikali imesema. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Kauli hiyo ilitolewa leo bungeni na Naibu Waziri wa Malisili na Utalii, Mohamood Ngimwa, alipokuwa akijibu swali la mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki, Dk.Luccy Nkya (CCM).

Katika swali lake Dk. Nkya alitaka kujua kujua ni lini serikali italipa fidia ya mazao yaliyoharibiwa na wananyamapori katika jimbo hilo kwa kuwa ni muda mrefu sasa tangu makadirio kupelekwa wizarani.

Aidha, alitaka kujua ni kwanini serikali haijalipa kifuta jasho kwa familia zilizopoteza mifugo na ndugu zao kutokana na mashambulizi ya samba na mamba.

Akijibu swali hilo, Mgimwa alisema kuwa kulingana na kifungu cha 68(1) cha sheria ya kuhifadhi wanyamapori Na 5 ya mwaka 2009, serikali hulipa kifuta jasho au kifuta machozi na si fidia.

Amesema hatua hiyo ni kwa mujibu wa kifungu cha 3 cha kanuni za malipo ya kifuta jasho au kifuta machozi za mwaka 2011. Kwamba, malipo yanafanyika endapo mwananchi atajeruhiwa au mazao yake kuharibiwa ama pale ambapo mifugo yake kuuliwa na wanyamapori.

Amesema kuwa malipo ya kifuta jasho au kifuta machozi hulipwa baada ya kufanyika tathmini kwa kufuata taratibu na kanuni zilizoainishwa.

Kwa mujibu wa Mgimwa, wizara imepokea maombi ya wananchi 65 kutoka katika vijiji sita ambapo jumla ya Sh. 5,368,000 zitalipwa.

error: Content is protected !!