Saturday , 20 April 2024
Home Kitengo Maisha Afya Mganga mkuu atoa tamko visa vya mafua, kikohozi, atahadharisha Corona kuongezeka
AfyaTangulizi

Mganga mkuu atoa tamko visa vya mafua, kikohozi, atahadharisha Corona kuongezeka

Mganga Mkuu wa Serikali, Dk. Aifello Sichalwe
Spread the love

 

WIZARA ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia Wazee na Watoto imesema kuongezeka kwa idadi ya watu wenye dalili za kukohoa, mafua, maumivu ya mwili na kuchoka, ni hali ya kawaida ya kila mwaka ambayo huchangiwa na mabadiliko ya hali ya hewa kama ambavyo imekuwa ikitokea kwa miaka mingine iliyopita. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Pia imewakuwakumbusha Watanzania kuwa ugonjwa wa UVIKO 19 unaosababishwa na virusi vya Corona bado upo na huenda maambukizi ya ugonjwa huo yakaongezeka hasa kuelekea mwisho wa mwaka unaohusisha kipindi cha msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka.

Imesema ni vema kuchukua tahadhari zote kama zinavyoelimishwa na wataalamu wa afya bila kusahau kuchanja.

Taarifa hiyo imekuja siku chache baada ya kuibuka wimbi la taarifa za watu wengi kuwa na dalili za kukohoa, mafua, maumivu ya mwili na kuchoka.

Taarifa iliyotolewa leo tarehe 18 Disemba, 2021 na Mganga Mkuu wa Serikali, Dk. Aifello Sichalwe inaeleza kuwa wizara pamoja na taasisi zake, zinaendelea kufuatilia kwa karibu viashiria vya mwenendo wa hali hiyo.

 

Imesema taasisi mbalimbali ikiwemo NIMR, vyuo vikuu na wataalamu kutoka wizarani, tayari wameelekezwa kuendelea kutoa takwimu na elimu kutokana na ufuatiliaji wa Kisayansi (Survellience) ambao wamekuwa wakifanya kuhusiana na Visa vya Mafua nchini.

Aidha, Wizara imeshauri wananchi wenye dalili hizi za kukohoa, mafua, maumivu ya mwili na kuchoka watoe taarifa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ili wafanyiwe uchunguzi wa kitaalamu na wapatiwe matibabu stahiki.

“Ndugu Wananchi, pamoja na hali hii ya mwenendo wa mafua ya kawaida, vilevile Wizara inaendelea kukumbusha na kutoa tahadhari kwa kila mtu kuendelea kuchukua hatua zote muhimu za kujikinga na janga la UVIKO-19 ikiwa ni pamoja kuepuka misongamano isiyokuwa ya lazima, kunawa mikono, kuvaa barakoa na kuhakikisha kuwa kila mtu anapata dozi kamili ya chanjo.

“Wito kwa wananchi kutoa taarifa za tetesi za viashiria vya magonjwa ya mlipuko kutoka katika jamii kupitia namba ya simu 199 bila malipo yoyote,” ilisema taarifa hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

error: Content is protected !!