June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mgambo 50 wavamia Ofisi ya Mkurugenzi Mwanza

Spread the love

ZAIDI ya Mgambo 50 wa Jiji la Mwanza waliosimamia mtihani wa Kidato cha Nne mwaka jana, wamevamia Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauli ya Ilemela wakishinikiza kulipwa fedha zao. Anaandika Moses Mseti.

Mgambo hao ambao wamekupo kwenye Ofisi ya Mkurugenzi, John Wanga kwa wiki moja sasa wakifuatilia maidai yao ya kiasi cha Sh. 20 milioni kutokana na kazi hiyo waliyoifanya bila malipo.

Wanga alipotafutwa kwa simu kuelezea sababu za mgambo hao kutolipwa pesa yao mpaka sasa, aligoma kuzungumza chochote.

Mgambo hao wamedai tangu Novemba mwaka jana, waliposimamia mtihani huo mpaka sasa hawajalipwa fedha zao na kwamba wamekuwa wakipigwa chenga na mkurugenzi.

Hata hivyo mgambo hao walidai kwamba, ofisa elimu wa sekondari, amekuwa akiwaeleza kuwa fedha zao zilitolewa lakini walipokwenda kwa mkurugenzi huyo aliwaeleza fedha hizo zimenunua gari la serikali.

Sagana Ikena, Elias Mayala kwa pamoja wametuhumu kuwa, Wilaya ya Ilemela imegubiwa na viongozi wababaishaji.

“Wilaya hii ni tatizo tena tatizo kubwa sana, tumeenda kwa DC (Mkuu wa Wilaya) katuandikia barua tuilete kwa mkurugenzi atulipe, kilifuata ametuitia askari polisi ambao walianza kututisha kwa silaha zao,” amesema Mayala.

Mayala amesema, baada ya kuendelea kuwabana viongozi hao kuhusu pesa zao, wajibiwa kwamba hakuna fedha za kuwalipa.

error: Content is protected !!