July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mfumuko wa bei wazidi kupaa

Bidhaa zikiwa sokoni

Spread the love

MKURUGENZI wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ephraim Kwesigabo ameutaarifu umma kuwa mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwezi Juni, 2015 umeongezeka hadi asilimia 6.1 kutoka asilimia 5.3 ilivyokuwa mwezi Mei ,2015. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Mfumuko huo wa bei, umetokana na baadhi ya bidhaa za vyakula na zisizo za vya kula kupanda bei hususani katika kipindi hiki cha mwezi wa ramadhani ambapo bidhaa nyingi hupanda bei hupanda bei.

Kwesigabo amesema, Fahirisi za bei zimeongezeka hadi 158.12 kwa mwezi juni, 2015 kutoka 148.98 mwezi juni, 2014. Ambapo, mfumuko wa bei kwa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi juni,2015 umeongezeka hadi asilimia 10.1 kutoka asilimia 8.5 ilivyokuwa mwezi Mei 2015.

Aidha, amesema kuongezeka kwa mfumuko wa bei hizo kwa mwezi Juni mwaka huu, kumechangiwa na kuongezeka kwa bei ya bidhaa za vyakula kama, mchele kwa asilimia 31.5, mahindi asilimia 8.1, unga wa muhogo, asilima 3.7, nyama asilimia 3.1, samaki asilimia 12.0 na maharage kwa asilimia 11.6.

Vingine, ndizi za kupika, kwa asilimia 2.3, matunda kwa asilimia 3.8, mbogamboga kwa asilimia 5.6, viazi mviringo kwa asilimia 4.9 na samaki kwa asilima 9.2.

Kwa upande wa bidhaa zisizo za vyakula, zilizochangia kuongezeka kwa mfumuko wa bei wa mwezi juni, 2015 ni pamoja na, mavazi ya wanaume, kwa asilimia 3.6, mavazi ya wanawake kwa asilimia 2.6, vyakula kwenye migahawa kwa asilimia 3.5 na huduma za malazi kwa asilimia 3.1, dizeli kwa asilimia 4.5 na mafuta ya petroli kwa asilimia 5.2.

Hata hivyo,Kwesigabo amesema, kuhusu thamani ya shilingi ya Tanzania mwezi Juni , 2015 uwezo wa shilingi 100 katika kununua bidhaa umefikia shilingi 63 na senti 24 mwezi Juni,2015, kutoka mwezi septemba,2010   ikilinganishwa na shilingi 63 na sent 35 ilivyokuwa mwezi Mei ,2015.

“Kwa ujumla mfumuko wa bei wa ndani unamwelekeo unaofanana na baadhi ya nchi za Afrika Mashariki kama Kenya na Uganda.

“Nitoe wito kwa wananchi wote kwa ujumla kutoa ushirikiano wa dhati kwa ofisi za Takwimu za mikoa wakati wa ukusanyaji wa Takwimu mbalimbali kwa lengo la kutoa taarifa zilizo sahihi kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu” amesema Kwesigabo.

error: Content is protected !!