January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mfumuko wa bei wazidi kuitesa Tanzania

Spread the love

OFISI ya Takwimu ya Taifa(NBS),  imetoa tathimini ya mfumuko wa bei mwezi Novemba ambapo umeongezeka kufikia asilimia 6.6 kutoka 6.3 mwezi Oktoba mwaka huu, Anaandika Faki Sosi…(endelea).

Akizungumza na waandishi wa  habari Jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Kijamii, Ephraim Kwesigabo, amesema kuwa mfumuko wa bei huo unaotokana na fahirisi za bei za bidhaa na huduma mbalimbali zinazotumiwa na kaya binafsi nchini.

Kwesigabo amesema kuwa fahirisi za bei zimeongozeka kutoka 159.17 mwezi oktoba kufikia 160.49 mwezi huu, ongezeko hilo limetokana kuongozeka kwa bei za vyakula ambapo bei ya mchele imeongezeka kwa asilimia 5.2, mahindi asilimia 5.4,unga wa ngano  asilimia 3.3 nyama asilimia 4.3 dagaa kwa asilimia 10.1 mbogamboga kwa asilimia  4.8,viazi mviringo kwa asilimiaa 10.4, na viazi  vitamu kwa asilimia 6.7.

Mfumuko wa bei kwenye nchi nyengine za Afrika Mashariki unafanana ambapo Kenya umefikia asilimia 7.32 mwezi novemba kutoka asilimia 6.72 mwezi Oktoba   ambapo Uganda umeongezeka kufikia asilimia 9.1 mwezi Novemba kutoka asilimia 8.8 mwezi oktoba.

Tanzania yenye asilimia chache zaidi ambazo ni 6.6 ,ambapo uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania kwa kununua bidhaa na huduma umefika shilingi 62 na senti  31  kwa mwezi Novemba.

error: Content is protected !!