January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mfumuko wa bei wafikia 4.5

Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ephraim Kwesijabo

Spread the love

MFUMUKO wa bei wa Taifa kwa Aprili mwaka huu, umeongezeka hadi asilimia 4.5 kutoka asilimia 4.3 ilivyokuwa Machi mwaka huu. Anaandika Pendo Omary … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa na Ephraim Kwesijabo – Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.

“Hii inamaanisha kuwa, kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia Aprili mwaka huu imeongezeka ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia Machi mwaka huu,” amesema Kwesijabo.

Kwesijabo amesema, Farisi za bei (kipimo kinachotumika kupima mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma mbalimbali zinazotumiwa na sampuli wakilishi ya kaya binafsi Tanzania), zimeongezeka hadi 157.21 kwa Aprili mwaka huu, kutoka Aprili, 2014.

Aidha, mfumuko wa bei na bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa Aprili mwaka huu, umeongezeka hadi asilimia 7.1 kutoka asilimia 5.9 ilivyokuwa Machi, mwaka huu.

“Kwa upande wa mfumko wa bei kwa bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula, badiliko la fahirisi za bei za bidhaa za vyakula nyumbani na migahawani limeongezeka hadi asilimia 7.2 Aprili mwaka huu, kutoka asilimia 6.1 Machi mwaka huu,” Kwesijabo ameeleza.

Pia, amesema badiliko la fahirisi za bei kwa bidhaa zisizo za vyakula limepungua hadi asilimia 1.0 Aprili mwaka huu, kutoka asilimia 2.0 Machi, mwaka huu.

Akielezea kuhusu mfumko wa bei wa bidhaa na huduma zote sipokuwa bidhaa za vyakula na nishati, Kwesijabo amesema “mfumko wa bei ambao haujumuishi vyakula na nishati kwa mwezi Aprili, mwaka huu, umepungua hadi asilimia 2.1 kutoka asilimia 2.5 Machi, mwaka huu.”

Fahirisi inayotumika kukokotoa aina hii ya mfumuko wa bei, haijumuishi vyakula vilivyoliwa nyumbani na migahawani, vinywaji baridi, petrol, dizeli, gesi ya kupikia, mafuta ya taa, mkaa na umeme.

“Mfumko wa bei wa Aprili, mwaka huu, unaopimwa kwa kipimo cha mwezi umeongezeka kwa asilimia 0.8 ukilinganisha na ongezeko la asilimia 0.7 Machi, mwaka huu. Fahirisi za bei zimeongezeka hadi 157.21 Aprili, mwaka huu, kutoka 155.88 Machi, mwaka huu,” amefafanua Kwesijabo.

Amesema, kuongezeka kwa fahirisi kumechangiwa hasa na kuongezeka kwa bei za bidhaa za vyakula. Baadhi ya bidhaa za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa fahirisi ni pamoja na mchele kwa asilimia 5.8 na mahindi kwa asilimia 6.3.

Bidhaa nyingine ni unga wa mahindi kwa asilimia 5.0 , samaki waliokaushwa kwa asilimia 3.1, maharage kwa asilimia 2.9, viazi mviringo kwa asilimia 7.0, mihogo kwa asilimia 6.4 na viazi vitamu kwa asilimia 4.0.

“Uwezo wa Sh. 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma umefikia Sh. 63 na senti 61 Aprili, mwaka huu, kutoka Septemba, mwaka huu,” amesema Kwesijabo.

error: Content is protected !!