July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mfumo wa kuhesabu kura wahojiwa

Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetaka kukaguzwa mfumo wa kuhesabu na kujumlisha kura utakaotumiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ili kuingia katika uchaguzi kwa maridhiano. Anaandika Hamisi Mguta … (endelea).

Chama hicho kimesema bila ya Tume kuruhusu mfumo huo uangaliwe na vyama vinayounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), inaweza kuja kutokea matatizo wakati utakapobainika unatoa mwanya wa uchakachuaji.

Wamesema kwamba wakibaini matatizo, hawatakuwa na la kufanya isipokuwa kutumia mfumo wanaojua unaleta ufanisi.

Hayo yameelezwa na Mwanasheria wa Chadema, John Mallya alipozungumza na waandishi wa habari leo kwenye kituo cha habari cha UKAWA, jengo jipya la LAPF Makumbusho.

Mallya amesema wameshapeleka barua kwa Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume hiyo kumjulisha kwamba wanahitaji kukagua mfumo huo, si hivyo hawapo tayari kukubali mfumo ambao hawajaukagua.

“Tumewaomba waturuhusu kupeleka wawakilishi wetu kwenda kufanya ukaguzi… na kama watakataa ombi letu, tutaendelea kuhesabu wenyewe kura zetu kwa mfumo wa kawaida kwa sababu haitakuwa demokrasia kutofahamu mfumo wa kuhesabu kura wakati wa uchaguzi,” amesema.

Mfumo wa kuhesabu na kujumlisha kura uliotumisa na Tume mwaka 2010, ulileta mtafaruku jimbo la Ubungo, na mgombea wa Chadema, John Mnyika, akalazimika kumshawishi aliyekuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Rajabu Kiravu, atumie mfumo waliouweka wao.

Kiravu alikubali baada ya kuukagua mfumo wa Chadema, na kazi ilikamilika kwa amani na salama. Mnyika alishinda ubunge.

error: Content is protected !!